Zawadi ya Ronaldo aliyozawadiwa na mkewe Georgina yakashifiwa kuwa "ponografia"

Mwanasiasa aliitaja kuwa kitendo cha filamu chafu kwa kuwa watu wengi wanakabiliwa na maisha magumu kutokana na mfumuko wa uchumi.

Muhtasari

• Iliarifiwa kuwa gari hilo la kifahari lina thamani ya  milioni 37 pesa za Kenya.

Ronaldo apewa zawadi ya gari la ifahari na mkewe
Ronaldo apewa zawadi ya gari la ifahari na mkewe
Image: Instagram

Siku moja baada ya sherehe za Krismasi, mpenzi wa nyota wa Ureno, Christiano Ronaldo, Georgina Rodriguez alimzawadi gari la kifahari aina ya Rollys Royce Phantom lililotajwa kuwa la thamani ya shilingi milioni 37 pesa za Kenya.

Huku mashabiki wake wakiendelea kumsherehekea kwa kupewa zawadi hiyo, jarida la Mirror limeripoti kuwa mwanasiasa mmoja nchini Uhispania aliikandia zawadi hiyo na kuiita kuwa ni ya kiponografia.

Kulingana na jarida hilo, mwanasiasa Miguel Angel Revilla alikuwa anazungumza katika mahojiano ya runinga ambapo alitaja kitendo cha Rodriguez kumzawadi baba wa watoto wake kama mchezo wa ponografia ambao watu hawafai kuchukulia kwa umakini wala uzito wowote.

Bw Revilla alirejelea matatizo ya kiuchumi ikiwa ni pamoja na mfumko mkubwa wa bei unaoathiri watu wengi kwa sasa kama alivyosema: "Nilidhani sasa ilikuwa ponografia. Kwa kile ambacho watu wanapitia kwa sasa, kwamba mambo haya yanatoka kwenye TV sio maadili. Mitazamo ya aina hii inaonekana kama ponografia ngumu."

Itakumbukwa kwamab hii si mara ya kwanza kwa Georgina kumpa Ronaldo zawadi ya gari  kwani mnamo Februari mwaka jana alipokuwa akisherehekea kufikisha miaka 37, alimzawadi gari jingine aina ya Cadillac Escalade lenye uwezo wa kubeba watu 8.

Mwanamitindo na mshawishi Georgina, 28, alichapisha zawadi ya kifahari ya Ronaldo kwenye Instagram Siku ya Krismasi, huku Rolls Royce ikiwa imefungwa kwa upinde mkubwa mwekundu.