Mount awaaga mashabiki wa Chelsea kabla ya kujiunga na Man United

Kwa sasa Mount anakaribia kujiunga na United katika mkataba wenye thamani ya pauni milioni 55 na anatarajiwa kutia saini mkataba wa miaka mitano ili kutua ugani Old Trafford.

Muhtasari

• Mount, ambaye alikuwa mhitimu wa akademia ya Chelsea, aliichezea Chelsea kwa takriban miaka 18 kuanzia alipo kuwa na umri wa miaka 6 pekee yake.

Mason Mount
Mason Mount
Image: GETTY IMAGES

Mason Mount aliwaaga mashabiki wa Chelsea siku ya Jumanne wakati mchezaji huyo wa  England akikaribia kuhamia mahisimu wakubwa wa timu yake ya zamani Manchester United.

Mount, ambaye alikuwa mhitimu wa akademia ya Chelsea, aliichezea Chelsea kwa takriban miaka 18 kuanzia alipokuwa na umri wa miaka 6 pekee yake.

Kwa sasa Mount anakaribia kujiunga na United katika mkataba wenye thamani ya pauni milioni 55 (bilioni 9.8 pesa za Kenya) na anatarajiwa kutia saini mkataba wa miaka mitano ili kutua ugani Old Trafford.

"Kutokana na uvumi uliokuwa ukienea mitandaoni katika kipindi cha miezi sita iliyopita, hii inaweza kuwa si jambo la kushangaza kwenu, lakini sio rahisi kusema kwamba nimefanya uamuzi wa kuondoka Chelsea," alisema katika video kwenye Instagram yake.

"Najua baadhi yenu hamtafurahishwa na uamuzi wangu lakini ndio jambo sahihi kwangu kwa wakati huu katika taaluma yangu."

Kiungo huyo alijiunga na Chelsea alipokuwa na umri wa miaka 6 na akawa kipenzi cha mashabiki baada ya kupandishwa daraja kutoka kuwa mchezaji wa akademia na kuwa mchezaji muhimu wa katika ushindi wa klabu hiyo wa Ligi ya Mabingwa mnamo 2021.

Mechazaji huyo mwenye umri wa miaka 24 aliweza kucheza mechi 195 na kufunga mabao 33. Alienda kutoka kwa kutajwa kuwa mchezaji wa mwaka wa klabu ya mwaka 2017, hadi kushinda tuzo ya mchezaji wa kwanza wa timu ya mwaka ya ligi kuu ya EPL katika 2021 na 2022.

Mount sasa anajiandaa kuanza sura mpya katika taaluma yake huko United, huku meneja Erik ten Hag akimfanya kuwa mlengwa muhimu kabla ya klabu hiyo kurudi kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.