'Ningependa Kumshuhudia Burna Boy akitumbuiza Live, Namkubali' - Harry Kane

Akiwa nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza, Kane alifichua kuwa wimbo mpya zaidi wa Burna Boy, "Big 7," unashikilia nafasi maalum kwake.

Muhtasari

• Mchezaji wa mpira wa miguu aliangazia athari za muziki wa Burna Boy, akisisitiza jinsi "Big 7" inavyoendana na mawazo ya kwake kila wakati anapoisikiliza.

Harry Kane na Burna Boy
Harry Kane na Burna Boy
Image: Instagram

Nahodha wa timu ya taifa ya UIngereza ambaye pia ni mshambuliaji anayekipiga zake kule Ujerumani kwa timu ya Bayern Munich, Harry Kane ameeleza kuvutiwa kwake na nyota wa Afrobeats, Burna Boy.

Mwanasoka huyo mwenye umri wa miaka 31 katika mahojiano ya hivi majuzi na ESPN UK, alifichua wimbo wake anaoupenda zaidi wa Burna Boy, na kuzua shauku miongoni mwa mashabiki wake.

Akiwa nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza, Kane alifichua kuwa wimbo mpya zaidi wa Burna Boy, "Big 7," unashikilia nafasi maalum kwake.

Mchezaji wa mpira wa miguu aliangazia athari za muziki wa Burna Boy, akisisitiza jinsi "Big 7" inavyoendana na mawazo ya kwake kila wakati anapoisikiliza.

Alipoulizwa kuhusu wimbo wa mwisho uliokwama kichwani mwake, Kane alijibu mara moja, “Unajua, ‘Big 7’ kutoka kwa Burna Boy? Ndio, napenda Burna Boy, kuwa sawa. Ilinijia kichwani tu pale.”

Kuhusu mwanamuziki huyo ambaye angependa kutazama maonyesho yao ya moja kwa moja, mshambuliaji wa zamani wa Tottenham alisema, "Labda mtu kama Burna Boy au Dave, unajua."

Burna Boy amekuwa akifanya vizuri katika malimwengu ya muziki huku pia Kane akiwa anafana na kupepea katika anga za juu kwenye masuala ya kandanda akiwa amefunga mabao mengi katika klabu yake mpya kwenye ligi ya Bundesliga.