Man Utd wameripotiwa kutaka kumnunua mchezaji aliyevurunda Chelsea, Timo Werner

Uamuzi wa The Blues kumuondoa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 ulikuja baada ya fowadi huyo kufanikiwa kufunga mabao 10 pekee ya Ligi Kuu katika zaidi ya mechi 50 za ligi kuu.

Muhtasari

• Iwe hivyo, inaeleweka kuwa hakuna ofa iliyotolewa na hakujakuwa na mazungumzo katika hatua hii.

Timo Werner
Timo Werner
Image: Facebook

Manchester United wamehusishwa na kutaka kumnunua aliyekuwa mchezaji wa Chelsea, Timo Werner kabla ya dirisha la usajili la Januari.

Mjerumani huyo alikaa miaka miwili kwenye Ligi ya Premia akiwa na The Blues, ambao alijiunga nao msimu wa joto wa 2020 kutoka kwa wababe wa Bundesliga, RB Leipzig.

Kulingana na Sportbible, miamba hao wa London Magharibi walilipa pauni milioni 47.5 kupata huduma ya mshambuliaji huyo.

Hata hivyo, baada ya kuhangaika sana Stamford Bridge, Chelsea walipunguza hasara na kumruhusu Werner kujiunga tena na Leipzig mnamo 2022 kwa pauni milioni 25.3 pekee.

Uamuzi wa The Blues kumuondoa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 ulikuja baada ya fowadi huyo kufanikiwa kufunga mabao 10 pekee ya Ligi Kuu katika zaidi ya mechi 50 za ligi kuu.

Hata hivyo, sasa imeibuka kuwa United wana nia ya kumrejesha nyota huyo wa Leipzig kwenye Ligi ya Premia.

Sky Germany inaripoti kwamba Mashetani Wekundu tayari wameuliza kuhusu upatikanaji wa mshambuliaji huyo kwa nia ya kumsajili kabla ya dirisha la usajili la Januari.

Iwe hivyo, inaeleweka kuwa hakuna ofa iliyotolewa na hakujakuwa na mazungumzo katika hatua hii.

Nia ya United kwa Werner inakuja wakati ambapo klabu hiyo inahitaji sana kuimarishwa zaidi kwenye safu yao ya ushambuliaji kutokana na ugumu ambao Marcus Rashford na Anthony Martial wamevumilia mbele ya lango.

Wakati Rasmus Hojlund amekuwa na mafanikio katika Ligi ya Mabingwa ya UEFA, ameshindwa kufanya alama kwenye ligi ya nyumbani.