Jurgen Klopp atajiuzulu kama meneja wa Liverpool mwishoni mwa msimu huu

"Ninaweza kuelewa kuwa ni mshtuko kwa watu wengi wakati huu, unapoisikia kwa mara ya kwanza," Klopp alisema.

Muhtasari

• Mameneja wasaidizi wa Liverpool Pepijn Lijnders na Peter Krawietz, pamoja na kocha wa ukuzaji wa wachezaji Vitor Matos, wataondoka katika klabu hiyo pamoja na Klopp.

Klopp ameshinda mataji sita makuu akiwa na Liverpool, ikiwa ni pamoja na Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa
Klopp ameshinda mataji sita makuu akiwa na Liverpool, ikiwa ni pamoja na Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa
Image: BBC

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp anatazamiwa kujiuzulu nafasi hiyo mwishoni mwa msimu huu, akisema "ameishiwa nguvu".

Klopp aliteuliwa Oktoba 2015 na mkataba wake ulipaswa kumalizika hadi 2026. Alishinda Ligi ya Mabingwa mwaka 2019 kabla ya kuiongoza Liverpool kutwaa taji lao la kwanza la ligi ya Primia baada ya miaka 30 mwaka 2019-20. "Niliiambia klabu tayari mwezi Novemba," alisema Klopp mwenye umri wa miaka 56, ambaye ametangaza uamuzi wake huku kikosi chake kikiwa kileleni mwa Premier League. 

"Ninaweza kuelewa kuwa ni mshtuko kwa watu wengi wakati huu, unapoisikia kwa mara ya kwanza, lakini ni wazi naweza kuielezea - ​​au angalau kujaribu kuielezea. 

"Ninapenda kila kitu kuhusu klabu hii, napenda kila kitu kuhusu jiji, napenda kila kitu kuhusu wafuasi wetu, napenda timu, napenda wafanyakazi. Ninapenda kila kitu. Lakini kwa kuwa bado ninachukua uamuzi huu inakuonyesha kwamba nina hakika, huu ndiyo uamuzi ninaopaswa kuchukua." 

Liverpool wameshinda kila taji kuu tangu Mjerumani huyo achukue mikoba ya Wekundu hao. Klopp aliiongoza Liverpool kutwaa Kombe lao la sita la Uefa mwaka 2019 walipoifunga Tottenham katika fainali ya Ligi ya Mabingwa mjini Madrid.

Walifuata hilo mnamo 2019-20 kwa ushindi Uefa Super Cup na Kombe la Dunia la Klabu la Fifa na, muhimu zaidi, kunyanyua taji la Ligi Kuu nchini Uingereza. Liverpool walishinda mataji ya nyumbani mara mbili msimu wa 2021-22, na walikosa mara nne baada ya kuzidiwa nguvu na Manchester City katika siku ya mwisho ya msimu wa Ligi Kuu na pia kupoteza fainali ya Ligi ya Mabingwa kwa Real Madrid huko Paris. 

The Reds walishindwa kushinda taji lolote kubwa msimu uliopita lakini wanawania mataji manne msimu huu. Waliifunga Fulham Jumatano na kutinga fainali ya Kombe la Carabao. 

Mameneja wasaidizi wa Liverpool Pepijn Lijnders na Peter Krawietz, pamoja na kocha wa ukuzaji wa wachezaji Vitor Matos, wataondoka katika klabu hiyo pamoja na Klopp. Mkurugenzi wa michezo Jorg Schmadtke ataondoka mwishoni mwa dirisha la uhamisho la Januari, baada ya kuteuliwa mwezi Juni.