Rashford awatolea uvivu wanaohoji kama anastahili kuendelea kuichezea Man Utd

“Hiyo ni kama mtu kuhoji kuhusu utambulisho wangu wote, na kila kitu ninachokiamini kama mwanamume. Nilikulia hapa, nimechezea klabu hii tangu nikiwa kijana" alisema.

Muhtasari

• “Mimi sio mtu mtimilifu, wakati ninafanya makosa, ninakuwa mtu wa kwanza kuinua mkono na kusema kwamba ninastahili kuboresha." alisema.

Rashford
Rashford
Image: Instagram

Winga wa Manchester United, Marcus Rashford ameamua kama mbwai na iwe mbwai tu!

Hii ni baada ya kuchoka kunyooshewa vidole vya lawama kutokana na kudorora kwa viwango vyake vya uchezaji msimu huu kaitka klabu yake ya Manchester United.

Rashford licha ya viwango vyake kudorora pakubwa msimu huu, bado meneja Erik Ten Hag amekuwa akimpa muda wa kucheza, jambo ambalo baadhi ya mashabiki na washikadau wanahisi halifai.

Baadhi ya wakosoaji wanahisi kwamba mchezaji huyo ni mzembe Zaidi kwenye kikosi na hastahili kuendelea kuitumikia Man United, lakini Rashford ameamua kuwajibu kwa maneno makali.

Akizungumza na Tribune, Rashford alisema kwamba mambo mengi yeye hunyamazia lakini linapokuja suala la kuhoji kujitolea kwake kwa Man United, hapo anahisi kuchokozwa kwani Man United ni kama baba na mama kwake.

“Mimi sio mtu mtimilifu, wakati ninafanya makosa, ninakuwa mtu wa kwanza kuinua mkono na kusema kwamba ninastahili kuboresha. Lakini ikitokea unaanza kuhoji kujitolea kwangu kwa Man United, hapo ndipo ni sharti nizungumze,” Rashford alisema.

“Hiyo ni kama mtu kuhoji kuhusu utambulisho wangu wote, na kila kitu ninachokiamini kama mwanamume. Nilikulia hapa, nimechezea klabu hii tangu nikiwa kijana, familia yangu ilikataa mkataba mnono wenye hela nyingi ili tu niwezwe kuichezea Man Utd,” Aliongeza.