Fahamu sababu ya mashabiki kuitaka klabu ya Chelsea kumtambua na kumuomboleza Mr Ibu

Katika mahojiano ya 2017, Mr Ibu alifichua kwamba binti yake wa pekee wa kumzaa alimpa jina "Chelsea" huku pia akifichua kwamba nyumbani kwake ameibandika jina "Stamford Bridge" - uga wa Chelsea FC.

Muhtasari

• Mkongwe huyo pia alifichua kwamba aliita nyumba yake baada ya uwanja wa nyumbani wa Chelsea, Stamford Bridge.

Mr Ibu
Mr Ibu
Image: X

Siku mbili baada ya kifo cha muigizaji mkongwe wa Nollywood John Okafor maarufu kama Mr Ibu kutoka Nigeria, baadhi ya mashabiki wa klabu ya Chelsea inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza wameiandikia timu hiyo barua.

Kwa mujibu wa barua hiyo, mashabiki hao wanaitaka Chelsea kumtambua rasmi Mr Ibu na kumuomboleza kabla ya kuanza kwa mechi yao wikendi ugani Stamford Bridge kwa kile wanataka kuwa alikuwa shabiki sugu kwa muda mrefu.

Mashabiki hao waliibua picha za zamani za Mr Ibu akiwa amevalia jezi ya The Blues na pia kufichua mahojiano yake ya awali akizungumza jinsi anavyoithamini timu hiyo katika moyo wake.

Kama ushahidi wa mapenzi yake kwa klabu hiyo ya London Magharibi, Bw Ibu, wakati wa mahojiano mwaka 2017, alifichua kwamba alimpa jina bintiye wa pekee wa kumzaa "Chelsea."

Mkongwe huyo pia alifichua kwamba aliita nyumba yake baada ya uwanja wa nyumbani wa Chelsea, Stamford Bridge.

“Naipenda Chelsea kwa damu yangu yote. Mke wangu alijifungua mtoto wa kike nje ya nchi. Hata kabla sijamuona mtoto wangu, tayari nilimpa jina la Chelsea. Yaani kukuambia…nyumbani kwangu, nyumba yangu inaitwa Stamford Bridge.”

Tazama video ya zamani kutoka kwa mahojiano ya Mr Ibu: