Liverpool waripotiwa kujiondoa katika mbio za kumchukua Xabi Alonso kumrithi Jurgen Klopp

Baada ya miaka mitatu kuinoa timu B ya Real Sociedad, Alonso alijiunga na Leverkusen mnamo Oktoba 2022, timu hiyo ikiwa katika nusu ya mwisho ya Bundesliga.

Muhtasari

• Bayern Munich pia walikuwa wanataka kumteua mchezaji wao wa zamani kama mbadala wa Thomas Tuchel anayeondoka.

XABI ALONSO
XABI ALONSO
Image: Hisani

Xabi Alonso hatarajiwi kuwa kwenye orodha ya walioteuliwa na Liverpool msimu huu wa joto, huku mchzaji huyo wa zamani wa Liverpool akitarajiwa kusalia Bayer Leverkusen.

Alonso aliaminika kulengwa sana kuchukua nafasi ya Jurgen Klopp, ambaye anaondoka Anfield mwishoni mwa msimu huu.

Bayern Munich pia walikuwa wanataka kumteua mchezaji wao wa zamani kama mbadala wa Thomas Tuchel anayeondoka.

Lakini kiungo huyo wa zamani wa Liverpool sasa anaaminika kusalia na Leverkusen, ambayo ameifikisha ukingoni mwa taji lao la kwanza la Bundesliga katika msimu wake wa kwanza kamili kama meneja.

Baada ya miaka mitatu kuinoa timu B ya Real Sociedad, Alonso alijiunga na Leverkusen mnamo Oktoba 2022, timu hiyo ikiwa katika nusu ya mwisho ya Bundesliga.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 42 aliunda uboreshaji uliopelekea kufuzu kwa Ligi ya Europa. Katika msimu wa pili wa Alonso, Leverkusen hawajashindwa katika mashindano yote na wanakaribia kumaliza utawala wa miaka 11 wa Bayern wa taji la Bundesliga.