Tukio la kipa Andre Onana kupaka Vaseline kwenye glovu wakati wa mechi lazua taharuki

Onana alionekana akipaka glovu zake mafuta wakati Liverpool ilikuwa ikipiga kona.

Muhtasari

•Kipa huyo mwenye umri wa miaka 28 alionekana akipaka mafuta ya Vaseline kwenye glovu zake katika dakika ya 33 ya mechi hiyo ya kusisimua. 

•Mchezaji wa zamani wa soka wa Australia Mark Bosnich alisema huenda kipa huyo aliyatumia kuongeza mshiko.

alionekana akipaka mafuta kwenye glovu wakati wa mechi dhidi ya Liverpool mnamo Aprili 7, 2024.
Kipa wa Manchester United Andre Onana alionekana akipaka mafuta kwenye glovu wakati wa mechi dhidi ya Liverpool mnamo Aprili 7, 2024.
Image: HISANI

Tukio la kutatanisha linalomhusisha mlinda mlango wa Manchester United Andre Onana lililotokea wakati wa mechi yao dhidi ya Liverpool kwenye uwanja wa Old Trafford siku ya Jumapili jioni limezua mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii.

Kipa huyo mwenye umri wa miaka 28 kutoka Cameroon alionekana akipaka mafuta ya Vaseline kwenye glovu zake katika dakika ya 33 ya mechi hiyo ya kusisimua. Hii ilitokea wakati Liverpool ilipokuwa ikipiga kona baada ya mlinda mlango huyo kuokoa shuti la Mo Salah na kuutuma mpira nje.

Tukio hilo sasa limezua mjadala mkubwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii huku watumiaji wengi wa mtandao wakihoji sababu halisi iliyomfanya mchezaji huyo wa zamani wa Ajax kupaka mafuta kwenye glovu zake. Hakika, ni tukio lisilo la kawaida katika uwanja wa mpira.

Picha na video za tukio hilo zimeenea kote na pia zimetumiwa kuunda meme za kuchekesha. Hii huenda ni kwa sababu mara nyingi Vaseline inahusishwa na shughuli nyingine zenye utata ambazo hakika si miongoni mwa madhumuni yaliyokusudiwa ya mafuta hayo.

“Je, kuna mtu anaweza kunieleza kama mtoto wa miaka 10, Kwa nini Onana alipaka Vaseline kwenye glavu zake wakati Manchester United ilikuwa inacheza na Liverpool jana?" Mtumiaji wa Twitter wa Kenya Omwamba aliandika Jumatatu asubuhi.

Katika juhudi za kujaribu kuelewa madhumuni ya mafuta hayo, mchezaji wa zamani wa soka wa Australia Mark Bosnich alisema huenda kipa huyo aliyatumia kuongeza mshiko.

"Kitu pekee ninachoweza kufikiria ni kwamba inamsaidia kushika mpira," Bosnich alisema wakati wa shoo kwenye Sky Sports News.

Akaunti maarufu ya Twitter inayojulikana kwa kuwakejeli wanasoka na vilabu vya soka, Troll Football, ilitania kuhusu Onana kutoweza kuudaka mpira kwa kupaka mafuta kwenye glovu.

"Onana alipaka Vaseline kwenye glavu zake, si ajabu kwamba hawezi kushika mpira," Troll Football aliandika.

Tazama maoni mengine kuhusu tukio hilo:

Pearl: Onana alinaswa akipaka Vaseline kwenye glavu na kuibua maswali ya uchezaji usio wa haki.

Ikechukwu Ude: Nilishangaa kuona kipa wa Manchester United Onana akipaka Vaseline kwenye glovu yake. Je, ni kipa wa aina gani anayetumia glavu inayoteleza kushika?

Guylord: Vaseline itapandisha mauzo yake kutokana na tangazo hili la bure kutoka kwa Onana mwenyewe.

AFYA CENTRE CREW: Sio Onana kupaka na Vaseline ili Liverpool waweze kupenya vizuri zaidi.

Im Just Woke: Andre Onana alionekana akiweka Vaseline kwenye glovu zake za goli dhidi ya Liverpool. Hakika, hilo haliwezi kuwa jambo bora zaidi kuweka mpira nje.

Dr Toolz: Onana anatakiwa kuacha kupaka Vaseline kwenye glovu zake ili aanze kudaka mpira.