Kenya PolicE kuchuana na KCB kwenye fainali ya kombe la Mozzart 23/24

Police fc wamejikatia tiketi ya fainali Jumatatu asubuhi baada ya kuwarindima AFC leopards 1-0.

Muhtasari

•Police FC itachuana na KCB baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya AFC leopards ugani Police Sacco Jumatatu asubuhi.

•Mechi hiyo ilisitishwa kutokana  vurugu kutokea Jumapili,huku mwamuzi msaidizi akijeruhiwa baada ya kurushiwa chombo na mashabiki.

Picha:Instagram
Picha:Instagram

Klabu ya Kenya Police FC imetinga kwenye fainali ya kombe la Mozzart baada ya kuwalabua Ingwe, kwenye nusu fainali iliyochezwa ugani Police Sacco Jumatatu asubuhi.

Mechi hiyo ambayo ilitatizika kwenye uwanja wa Police Sacco kutokana na kuumia kwa refa msaidizi wa pili, Samuel Kuria, iliendelea tena Jumatatu, Mei 27.

Kuria alipata jeraha baada ya kugongwa na chombo kilichorushwa na mashabiki, na kusababisha mechi hiyo kusimamishwa katika dakika ya 60.

Licha ya jitihada za kuendelea na mchezo huo baada ya tukio hilo kudhibitiwa, kukosekana kwa mwangaza kwenye eneo la tukio kuliibua wasiwasi mkubwa wa kiusalama na kusababisha mechi hiyo kuahirishwa.

Aidha mechi iliendelea Jumatatu asubuhi kwa dakika thelathini.Tito Okello aliwaweka mbele Police FC kwenye dakika 60 zilizochezwa Jumapili.

Police FC watamenyana na KCB kwenye fainali huku AFC leopards na Kariobangi Sharks wakiwania tatu na nne bora.