Chelsea yamteua Maresca kama kocha mpya

The Blues wamempa Enzo Maresca kandarasi ya miaka mitano na chaguo la nyongeza ya mwaka.

Muhtasari

•Muitaliano huyo anachukua nafasi ya Mauricio Pochettino, ambaye aliondoka kwa makubaliano tarehe 21 Mei baada ya msimu mmoja tu Stamford Bridge.

Enzo Maresca
Image: HISANI

Chelsea wamemteua mkufunzi wa Leicester Enzo Maresca kama kocha wao mpya kwa kandarasi ya miaka mitano na chaguo la nyongeza ya mwaka.

Muitaliano huyo anachukua nafasi ya Mauricio Pochettino, ambaye aliondoka kwa makubaliano tarehe 21 Mei baada ya msimu mmoja tu Stamford Bridge.

Maresca, 44, alichukua jukumu la kuinoa Foxes mnamo Juni 2023 na kuwaongoza kuchukua ubingwa msimu uliopita

"Kujiunga na Chelsea, moja ya klabu kubwa duniani, ni ndoto kwa kocha yeyote," alisema. "Ndio maana nimefurahishwa sana na fursa hii.

"Ninatarajia kufanya kazi na kundi la wachezaji na wafanyikazi wenye vipaji ili kukuza timu ambayo inaendeleza utamaduni wa mafanikio wa klabu na kuwafanya mashabiki wetu wajivunie."

Maresca, ambaye ataanza kazi yake mpya Julai 1, ni kocha wa Chelsea katika kipindi cha miaka mitano na wa nne tangu mwekezaji Mmarekani Todd Boehly na kampuni ya hisa ya Clearlake Capital kuinunua klabu hiyo Mei 2022.