Havertz ammiminia sifa tele kocha wake,Mikel Arteta.

Havertz alikabiliwa na ukosoaji katika miezi ya mwanzo ya wakati wake Arsenal, akijitahidi kuleta ubora,hii ikiwa ni changamoto ambayo anajivunia kushinda.

Muhtasari

•Kai Havertz amemtaja Mikel Arteta kama baadhi ya wakufunzi bora ulimwenguni kutokana na uzoefu wake wa kufichua mbinu mbalimbali za kutumia wakati wa mechi.

•Mshambulizi huyo alijiunga na Arsenal mwaka jana kutoka Chelsea kwa pauni ya milioni 65.

 

Image: INSTAGRAM// KAI HAVERTZ

Kai Havertz amemsifu mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta kama "fundi bora zaidi" ambaye amewahi kufanya naye kazi baada ya msimu mzuri wa kwanza akiwa na The Gunners.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani alikabiliwa na ukosoaji katika miezi ya mwanzo ya wakati wake kaskazini mwa London, akijitahidi kuleta ubora   kwenye uwanja.Hii ikiwa ni changamoto ambayo anajivunia kushinda.Havertz alifunga mabao tisa katika miezi minne ya mwisho ya msimu, akifanya vyema katika nafasi ya mbele.

"Haikuwa rahisi pia kwa Arsenal mwanzoni,” Havertz aliambia  waandishi wa gazeti la Welt am Sonntag kule Ujerumani.

"Mashabiki wa Chelsea walikuwa na hasira kwamba niliondoka, na mashabiki wa Arsenal walikuwa na shauku pia kwa sababu mambo hayakuwa sawa mwanzoni. Unapata nguvu wakati kocha, wachezaji wenzako, na watu wa karibu wako wakisimama karibu na kukuunga mkono.”

 Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 aliangazia ubora wa Mikel Arteta  kwa maelezo yake   kama chanzo cha mafanikio yake kwenye soka.

"Kuhusu jukumu lake kama kocha wa klabu, sijawahi kuwa na mtu bora zaidi katika masuala ya mbinu. Anakupa majukumu hadi maelezo ya mwisho na kuwasilisha masuluhisho ya kile kinachokaribia kutokea uwanjani.Hii inaonekana haswa kuhusiana na timu yetu changa huko Arsenal kwa sababu sio kila timu changa ina muundo mzuri kama sisi. Inashangaza kuona jinsi Arsenal ilivyokua chini yake kwa miaka minne.”

Arsenal wamehusishwa na mshambuliaji wa Sporting Viktor Gyokeres na nyota wa RB Leipzig Benjamin Sesko, huku gazeti la LondonWorld likiripoti kwamba Sesko analengwa na Arteta msimu huu wa joto ili kuimarisha ushambulizi .