Terzic aondoka Dortmund kama kocha mkuu

Terzic ameweka rekodi ya kushinda mara 55 kati ya michezo 96, baada ya kuisaidia timu hiyo kubeba kombe la DFB 2020/21 na kufika fainali ya UEFA mwaka huu.

Muhtasari

•Edin Terzic ameondoka Dortmund baada ya kuitaka klabu hiyo kukatisha mkataba wake mara moja.

•Kocha huyo aliwezesha Dortmund kufika fainali ya ligi ya mabingwa 2023/24 kabla ya kupoteza dhidi ya Real Madrid.

Kocha wa Dortmund
Edin Terzic Kocha wa Dortmund
Image: Ghetty images

Edin Terzić ameacha nafasi yake kama kocha mkuu wa Borussia Dortmund licha ya kuiongoza timu hiyo hadi fainali ya ligi ya mabingwa mwezi uliopita.

Terzic, 41, amekuwa na Dortmund katika majukumu mbalimbali tangu 2018, akiwa pia alitumia miaka mitatu kufanya kazi katika uanzishaji wa vijana kabla ya kuwa msaidizi wa Slaven Bilic kule Besiktas na West Ham United kati ya 2013 na 2017.

Hivi majuzi, aliisaidia klabu hiyo kufika fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya, ambapo walishindwa kutamba mbele ya Real Madrid, lakini Terzic sasa amethibitisha kwamba safari yake na Dortmund haitaenda mbali zaidi.

"Wapenzi mashabiki wa Borussia, ingawa inaniumiza sana hivi sasa, ningependa kuwaambia kwamba nitaondoka BVB leo," Terzic alisema katika taarifa yake.

Mkurugenzi mkuu mtendaji wa Dortmund Hans-Joachim Watzke alimsifu Terzic na kumtaja kama baadhi ya kocha bora.

"Edin Terzic amefanya kazi nzuri sana wakati alipokuwa BVB. Sote tunadaiwa deni kubwa la shukrani. Edin na mimi tutabaki marafiki daima."Hans-Joachim alisema.

Terzic anamaliza muda wake wa miaka miwili kama meneja akiwa na rekodi ya kushinda mara 55 kati ya michezo 96, baada ya kuisaidia timu hiyo kubeba Kombe la DFB 2020/21 pia.

 Ripoti zinaonyesha kuondoka kwa Terzic kunaweza kuwa na athari kubwa kwa mustakabali wa beki wa kati Mats Hummels,ambaye mkataba wake unamalizika msimu huu wa joto na, kulingana na Sky Sports Germany, alikuwa tayari kufikiria kuongeza muda ikiwa Terzic ataondoka katika klabu hiyo.