Shabana FC kucheza mechi 5 nyumbani bila mashabiki kwa kuzua rabsha mechi ya wikendi jana

“Kwamba Shabana FC itacheza mechi zake tano (5) za nyumbani bila mashabiki kuanza na mchezo wao wa nyumbani dhidi ya Posta Rangers Jumamosi Septemba 28, 2024" FKF ilisema.

Muhtasari

• “Kwamba Shabana FC itacheza mechi zake tano (5) za nyumbani bila mashabiki kuanza na mchezo wao wa nyumbani dhidi ya Posta Rangers Jumamosi Septemba 28, 2024" FKF ilisema.

MASHABIKI WA SHABANA
MASHABIKI WA SHABANA
Image: X//SHABANA-FC-KENYA

Klabu ya soka ya Shabana FC wamepigwa marufuku ya kushiriki mechi zao 5 zijazo nyumbani za ligi kuu nchini FKF-PL kufuatia fujo zilizoshuhudiwa baada ya mechi yao dhidi ya Ulinzi Stars wikendi jana.

Bodi ya nidhamu ya shirikisho la soka nchini FKF ilitoa uamuzi huo baada ya kutathmini uharibifu uliosababishwa na mashabiki wa Shabana baada ya sare ya 2-2 dhidi ya Ulinzi ugani Ulinzi Sports Complex.

“Shabana FC ilikiuka Kanuni ya 9.3.3 ya Sheria na Kanuni zinazosimamia Soka ya Kenya (2019) ambayo inasema: “Vilabu vinawajibika kwa mienendo ya wanachama na wafuasi wao na lazima vihakikishe vinatenda kwa haki na kujiepusha na vurugu. , vitisho, matusi, matusi na tabia nyingine za uchochezi na zisizo za kimichezo kwenye mechi” FKF walisema.

Kufuatia ukiukaji wa kanuni hizo, FKF ilitamka marufuku ya mashabiki uwanjani kwa mechi 5 pamoja na kugharamia matibabu ya waliojeruhiwa lakini pia ukarabati wa vitu vilivyoharibiwa uwanjani Ulinzi Complex.

“Kwamba Shabana FC itacheza mechi zake tano (5) za nyumbani bila mashabiki kuanza na mchezo wao wa nyumbani dhidi ya Posta Rangers Jumamosi Septemba 28, 2024. Klabu itakuwa na jukumu la kuhakikisha kwamba wafuasi wake wanafuatwa na adhabu hii.”

“Kwamba Shabana FC italipa fidia/itachukua gharama ya viti vilivyoharibika katika Ulinzi Sports Complex. Kwamba Shabana FC itatoa fidia kwa gharama za matibabu zilizotumiwa na maafisa wawili waliojeruhiwa. Ulinzi Stars FC itatoa stakabadhi zinazohitajika za gharama zitakazolipwa na klabu,” uamuzi huo ulisoma kwenye tovuti ya FKF.