Tazama orodha mpya ya FIFA ya timu 20 bora Duniani baada ya Kombe la Dunia

Licha ya kushinda Kombe la Dunia, Argentina imeorodheshwa ya pili.

Muhtasari

•Brazil wamesalia kileleni licha ya kubanduliwa nje ya Kombe la Dunia katika hatua ya robo fainali.

•Ufaransa wamepanda kutoka nafasi ya nne hadi ya tatu huku Ubelgiji wakishuka ngazi mbili hadi nafasi ya nne.

Argentina waliibuka washindi wa Kombe la Dunia 2022.
Image: INSTAGRAM// LIONEL MESSI

Argentina imepanda kutoka nafasi ya tatu hadi nafasi ya pili kwenye orodha ya timu bora za soka duniani baada ya kushinda Kombe la Dunia nchini Qatar siku ya Jumapili, sasa imefichuliwa.

Kulingana na orodha mpya ya FIFA iliyoratibiwa kutolewa rasmi siku ya Alhamisi, mahasidi wao wakubwa Brazil wamesalia kileleni licha ya kubanduliwa nje ya Kombe la Dunia katika hatua ya robo fainali.

Washindi wa pili wa Kombe la Dunia 2022, Ufaransa wamepanda kutoka nafasi ya nne hadi ya tatu huku Ubelgiji wakishuka ngazi mbili hadi nafasi ya nne. Uingereza imesalia katika nafasi ya tano.

Hii hapa orodha ya timu bora 20 mwaka wa 2022:-

1) Brazil

2) Argentina (+1)

3) Ufaransa (+1)

4) Ubelgiji (-2)

5) Uingereza

6) Uholanzi (+2)

7) Croatia (+ 5)

8) Italia (-2)

9) Ureno

10) Uhispania (-3)

11) Moroko (+11)

12) Uswizi (+3)

13) Marekani (+3)

14) Ujerumani (-3)

15) Mexico (- 2)

16. Uruguay (-2)

17. Colombia

18. Denmark (-8)

19. Senegal  (-1)

20. Japan (+4)