Msanii Willy Paul atoa msamaha wake kwa Rayvanny, asema 2020 sio ya bifu tena

vanny
vanny
Msanii Willy Paul ametangaza kukomesha bifu na staa wa bongo Tanzania Rayvanny.

"Tag this guy.. ajione song ilivo kuwa kubwa.. big up to everyone one kwa support yenu..  I dont want to end the year with grudges manze. God said, learn to forgive right? So haijalishi nini ama nini. Wacha kazi iendelee.. this song is still a masterpiece manze. Big up brother.. .." Alichapisha Willy Paul.

Kulizuka hali ya kutoelewana kati ya wasanii hawa huku Willy Paul akimlaumu Rayvanny kwa wizi wa ngoma ya Chuchuma.

Pozze alidai kuwa ubunifu wa ngoma ya Chuchuma ulikuwa wa kwake kutoka mwanzoni.

Wasanii hawa walikuwa na mpango waifanye pamoja ila kukawa na kutoelewana.

Baadaye Rayvanny aliimba ngoma hiyo na nyota wa kike Nora Fatehi.

Collabo ya Rayvanny na Fatehi ilifanya vizuri katika mtandao wa You Tube ikilinganishwa na yake Willy Paul.

"Alibadilisha kila kitu katika ile nyimbo. Nikakataa. Halafu nikawa nafikiria hilo ni tatizo ndogo ambalo hatufai kuwa nalo. Sisi ni mandugu, urafiki wetu unafaa kwa wa kwanza. Tuendelee kuwa marafiki ila nitafanya nyimbo yangu kwa sababu naipenda jinsi ilivyo." Alisema Pozze.