Mwanamke awauwa watoto wake na mumewe Roysambu

62641698_463272904490540_919535522788778366_n (1)
62641698_463272904490540_919535522788778366_n (1)
Mwanamke mwenye umri wa kati kutoka Thome Estate huko Roysambu, kata ya Nairobi, siku ya Jumatatu, aliwaua mumewe na wana wake wawili.

Polisi wanaamini kwamba mwanamke huyo alimdunga mumewe na kumnyoga bintiye mwenye umri wa miaka 3 na kijana wa miaka 5 kabla ya kujiua kwa sababu zisizojulikana.

Naibu wa OCPD wa Kasarani, Catherine Ringera, alisema kuwa mwanamke huyo alijinyonga baada ya kuua familia yake.

Polisi walisema watachunguza zaidi ili kubainisha kama watu wengine walihusika katika vifo hivyo.

Polisi walipata kisu na shoka zililoloa damu kwenye eneo la tukio la uhalifu.Majirani walidai mara nyingi mwanamke huyo alimdhulumu mumewe wakati walipokuwa na migongano.

Mwanamke huyo alijaribu kusafisha silaha zilizotumika kutekeleza mauaji yale kabla ya kuyachukuwa maisha yake, polisi wanasema.