Mzazi aliyeshtaki shule ya Rusinga kortini kwa kumfurusha mwanawe kwa sababu ya nywele rasta apoteza kesi hiyo

Mzazi wa mvulana wa umri wa miaka sita aliyeshtaki shule ya Rusinga mahakamani kwa kumfukuza mwanawe kwa sababu ya nywele rasta amepoteza kesi aliyowasilisha kortini akitaka shule hiyo iamuriwe kumkubali mwanawe arudi shuleni.

Jaji katika kesi hiyo, Mumbi Ngugi, alisema katika uamuzi wake kuwa mwanafunzi huyo itabidi anyoe nywele hizo ama atafute shule ingine kwa sababu mama yake hakuweza kushawishi mahakama kuwa alikuwa anafunga nywele hizo kwa sababu za kidini. Jaji Mumbi aliongezea kuwa mzazi huyo alikuwa amesoma na kutia saini kanuni za maadili ya shule hiyo kwa hivyo alikuwa na ufahamu kuwa wanafunzi hawakubaliwi kufuga nywele ya aina ya rasta.