Nabii Yohana Kutoka Bungoma Awaandikia Wanasiasa Barua Akionya Kuwepo Na Giza Nchini

prophecy
prophecy
Jamaa mmoja kutoka kijiji cha Nandolia eneo bunge la Kanduyi kaunti ya Bungoma anayedai kuwa Nabii wa tano ameandika barua akidai kuwa kutakuwa na Giza hivi karibuni nchini.

Nabii Yohana wa tano amewaandikia viongozi wa kisiasa na kanisa la kikatoliki nchini barua ya kuwaalika nyumbani kwake ili kuwapokeza ujumbe ambao ni muhimu kwa taifa la kenya

Kwenye barua yake, amewaonya viongozi wakiwemo Rais naibu wa rais, maseneta, magavana waache kugawanya wakenya kwenye misingi ya kisiasa na jamii kwa jumla

Nabii huyu vilevile anakumbukwa kwa kuandika bibilia yenye jumla ya vitabu 90 akiwa na wake thelathini na sita na watoto tisini.

Yohana amesema tarehe ishirini na sita mwezi huu ndiyo tarehe viongozi hao wanatakiwa kufika katika boma lake la Nandolia huko Bukembe kaunti ya Bungoma.

-Brian Ojamaa