KQ

Ni Kubaya!KQ yawatuma wafanyikazi kwa likizo ya bila malipo kabla ya awamu nyingine ya kuwachisha kazi

Shirika la safari za ndege  nchini Kenya Airways  limewataka wafanyikazi wake  ambao huduma zao hazihitajiki linaporejelea oparesheni zake kuchukua likizo ya  bila malipo .

Afisa mkuu mtendaji wa shirika hilo  Allan Kilavuka amesema  maelekezo hayo yanaanza kutekelezwa julai tarehe 6 .

Kupitia taarifa kwa wafanyikazi wake KQ imewataka wale ambao huduma zao hazitahitajika kwa sababu hapatakuwa na shughuli  nyingi za usafiri kuchukua  likizo hiyo ya bila malipo kuanzia julai tarehe sita .

Uhuru ahamia Jumba la Harambee kutoka Ikulu kwa ajili ya COVID 19

Amesema uamuzi huo umechukuliwa ili kuwapa fursa ya kuzungumza na washirika pamoja na wadau wengine kuamua hatua bora zaidi kwa wafanyikazi wa shirika hilo na kampuni nzima .

“ Ingawaje sote tumeweka juhudi kabambe za kuhakikisha kwamba tunaendelea na biashara yetu ,hali imekuwa ngumu na changamoto zilizopo ni nyingi kuendelea na  oparesheni zetu’ amesema afisa huyo mkuu

Matiang’i: Kenya iko tayari kurejelea usafiri ndani na nje ya nchi

Amesema tathmini yao imeeleza kwamba itawalazimu kupunguza idadi ya wafanyikazi  hata wanapoanza kurejelea oparesheni baada ya sekta nzima ya usafiri wa angani kuvurusgwa pakubwa na  janga la corona .

Kilavuka amesema kwa ajili ya uhaba wa watu wanaosafiri ndege zao nyingi zitasalia bila shughuli na hivo basi wafanyikazi wengi hawatahitajika .

 

 

 

Photo Credits: Hisani

Read More:

Comments

comments