Kipchoge-hugging-his-wife

‘Ni mwiko!’Sababu ya Kipchoge kutosafiri na mke wake kwa mashindano za mbio

Jamaa mmoja kutoka kwenye kaunti anakotoka Kipchoge, Kaunti ya Nandi alisema kuwa amekereketwa maini sana na madai ya watu wanaosema kuwa bingwa Eliud Kipchoge hakumkumbatia mke wake vizuri baada ya kumaliza mbio za Ineos.
Bwana Eliud Kipchoge alikuwa mwanaume wa kwanza kumaliza mbio kwa muda wa chini ya masaa mawili.
Eliud Kipchoge
Hata hivyo,vile tujuavyo,kwa kila kitu kizuri kuna kitu ambacho watu bado watatafuta kosa na kulikosoa .

Jamaa huyu kutoka kaunti ya Nandi alisema kuwa,

“Kwani mashabiki walikuwa wanataka amkumbatie aje mke wake ilhali bwana huyu alikuwa anakimbia kwa kasi sana.Wakenya mnapenda mambo madogo sana.”

Vilevile, alizidi kusema kuwa,

Miili ya Mariam na mwanawe yapatikana ikiwa imekumbatiana

”Bibi yake Kipchoge hafai kusafiri na yeye.Kitambo tulikuwa tunabaki na mke Kipchoge Eldoret na kutizama runinga huku tukimshangilia Kipchoge akiwa mbioni”

Eliud Kipchoge

Zaidi ya hayo,Bwana huyu Captain Kale alizidi kusema,

”Katika mila na desturi za wa Nandi ni mwiko mkubwa sana kutokimbia ukikutana  na mwanamke njiani.Endapo umekutana na mwanamke,unafaa kukimbia mbio sana.

(+Video yavuja) Mariam Kighenda akicheza Kainama ya Harmonize kabla ajali Likoni Feri

Huwa tunasema kuwa,unapoenda kuwinda ama kazini,hufai kumbeba mke wako na kuenda naye.

Kama Kipchoge angekuwa anambeba bibi yake kila wakati anapoenda kwenye mbio hizi,hangekuwa amefika alipo sasa.”

Captain alizidi kusema kuwa,wanaume katika ukoo huu huwa hawaishi na wake wao.

Mwisho kabisa,Captain Kale aliwaambia mashabiki,

Tafadhali msituharibie raha tuliyo nayo kwa sababu ya mambo madogo.Wacha tuendelee kusherehekea.

 

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments