Niacheni ! Naomba utulivu niomboleze mume wangu, Ruth Mueni

Screenshot_from_2019_12_12_13_31_46__1576146740_44230
Screenshot_from_2019_12_12_13_31_46__1576146740_44230
Mkewe marehemu John Mutinda amezitaka vyombo vya habari kumpa amani na wakati mtulivu wa kuomboleza mwanawe.

Kisa cha John kujitosa na kufa maji Bahari hindi kilingonga vichwa vya habari huku wengi wakiwa na lengo la kujua sababu zilizochangia marehemu kujiua.

Ndoa ya marehemu na mkewe Ruth Mueni inasimuliwa kuwa na matatizo yanayokisiwa kuwa yalichochea kujitoa uhai.

Katika mahojiano na vyombo vya habari mama huyu amesema kuwa ana imani kuwa mwanawe alijiua.

Aidha, mamake amisema kuwa mwanawe alikuwa anauguza majeraha ya kuchomwa kwa maji moto.

Mkewe John Mutinda aidha alizitaka vyombo vya habari kumkoma ili apate nafasi tulivu ya kumuomboleza mumewe.

Mwili wa mwendazake ulitolewa baharini saa mbili na dakika arobaini asubuhi siku hiyo hiyo.

Mamlaka ya huduma za feri nchini ilisema kuwa gari lake liliopolewa mwendo wa saa sita mchana.

Gari hilo lilipatikana mita 6 chini ya bahari Hindi.