PATANISHO: Nilikosana na mke wangu baada ya kupenda mhudumu wa klabu

Katika kipindi cha patanisho mwanamume kwa jina Simon Kithaka,37, kutoka Embu alituma ujumbe apatanishwe na mkewe Rose Wambui mwenye umri wa miaka 32, ambaye ni polisi wa utawala waliyekosana naye miezi miwili iliopita.

Wawili hao wamekuwa katika ndoa kwa miaka minane, Simon alikiri kuwa walikosana kwa sababu yeye mwenyewe alianza kuwa na uhusiano wa nje ya ndoa.

"Tumebarikiwa na watoto wanne nilikosana na mke wangu kwa ajili nilienda nje ya ndoa, ilikuwa mwaka jana krismasi ambapo nilienda kujivinjari na marafiki. Tulilewa lakini kuna mwanamke ambaye alikuwa ananikoroga akili, nilikuwa nampenda na yeye alinipenda, lakini katiba sikusoma." Simon Alieleza

Mke wake Simon alikuwa na haya ya kusema.

"Kwa kweli mimi nimemsamehe Simon kutoka kwa moyo wangu lakini kurudi sitarudi, alimleta huyo mwanamke nyumbani mwangu.

Kwanza hata kwa shamba ambalo nilinunua, mimi mwenyewe nilitoka huko na nikamuachia shamba lenyewe sikuchukua hata kijiko nimemuachia.

Wacha aendelee na maisha yake na aniwache niendelee na maisha yangu, nataka tu aniruhusu nije nichukue sare zangu za kazi pekee.

Sikutarajia kama anaweza kujishusha hadi kiwango hicho." Rose Alizungumza.

Simon hakubanduka alijitetea na kusema,

"Kama amenisamehe, hataki kurudi kwanini, arudi tu asiniharibiye kura zangu za mwaka wa 2022, wawania kiti cha MCA." Alisema.

Rose  alisema hatorudi tena katika ndoa yake.