PATANISHO: Gidi Hii Nayo Ukiweza Nakununulia Soda

Mama Brian alituma ujumbe ambaye walikosana mwezi wa nne.

"Tumefungua duka la dawa pamoja na sasa kuna siku nilienda kwa duka nikampata na mwanadada fulani na jinsi walivyokuwa wameketi nikawashuku sana.

Sasa kwa hasira nikawarushia cheche za matusi na hapo mume wangu akakasirika na kutoweka nyumbani, alipoelekea na kufungua duka lake la dawa kwao nyumbani.

Jinsi walivyokuwa wameketi haikuwa kawaida ya mgonjwa na daktari kwani walikuwa wameketi nikama kuna kitu kilikuwa kinaendelea. Gidi ukifaulu kumzungumzia nitakununulia soda." Alijieleza.

Wawili hao wana mtoto mmoja katika ndoa ya miaka mitano.

Alipopigiwa simu baba Brian alikiri kuwa yuko kazini na hangeweza kuzungumza nasi.

"Aliniomba msamaha na tayari nimemsamehe na uamuzi niliofanya ni kuwa hatuwezi rudiana na yeye pia anafaa kuishi hivo." Alijieleza Baba Brian kabla ya kukata simu pindi tu aliposkia sauti ya aliyekuwa mkewe.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be