PATANISHO: Mke wangu ameninyima tendo la ndoa kwa wiki tatu

Jackson, 39, aliomba apatanishwe na mkewe, bi Margaret, 33, ambaye walikosana wiki tatu zilizopita na tangia wakti huo, hataki kufanya mapenzi nawe.

"Shida yake alianza kununa nuna tu ananiambia maneno ambayo sielewi na mimi wakati mwingine nikija nyumbani huwa nimechoka na sikuwa naweza kushiriki tendo la ndoa naye.

Sasa na mimi nikitaka tendo hilo hataki." Alisema Jackson, akisema kuwa alimtuma dadake kumuuliza mkewe shida iko wapi na alimuambia kuwa yeye hampi fedha za pocket money.

Aliongeza kuwa haoni kama hilo ndio sababu kwani yeye humpa chochote anachotaka na mkewe anaelewa aina ya kazi yake.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka kumi na tatu na wamejaliwa watoto.

Alipopigiwa simu bi Margaret ambaye ni shabiki sugu wa Radio Jambo alisema wawili hao walikuwa wamezungumza na mumewe akasema hana shida na wakamaliza hayo maneno.

"Gidi, kuna mambo mengi mzee wangu hunifanya, la kwanza tumetoka mbali kama ni mifugo tumechuma kwa pamoja na sahii tunaeza sema tuko at least.

Huyu bwana wa watoto wangu tangu tuoane 2006 hajawahi toa hata shilingi na husema kuwa hatawahi toa mahari." Alisema Margaret akiongeza kuwa hata mafuta ya kujipaka hanunuliwi.

Maneno ya tendo la ndoa ni kwa sababu niliskia alilala na dadake mwenyewe miaka mitatu na hiyo kitu huwa na uchungu nayo. Huyu msichana alikuwa rafiki wangu wa dhati na kuna wakati nilipata message ikisema 'mbona sikuoni' saa sita ya usiku. Aliongeza.