PATANISHO:Nataka kualikwa harusi sio kupatanishwa! Lucy amwambia Wanjala

Yamempata Wanjala mwenye umri wa miaka 25 ambaye  leo ametaka kupatanishwa na  mpenzi wake wa zamani Lucy aliye na umri wa miaka 22.

Baada ya miaka mitano bila kupata mtoto wawili hao waliamua kutafuta usaidizi wa mamake Lucy aliyempeleka kwa shangazi yake kufanyiwa tambiko ili apate mtoto. Lakini matumaini yao ya kumpata mtoto yalitibuka wakati siku moja Lucy  alipotoroka nyumbani .

Wanjala anasema huenda Lucy alichochewa na watu kwamba , alikuwa na mke mwingine. Alipopigiwa simu, Lucy alikataa katu kurudiana na Wanjala akisema tayari ashachukua uamuzi mwingine. Lucy ana hamaki sana  kwa sababu wakati mmoja Wanjala alimwambia kwamba ashapata mke mwingine .

Amefanya ucheshi sana mwanadada huyo kwa kushangazwa na hatua ya  kupigiwa simu na Gidi  na Ghost kupatanishwa  akisema –

"Nilifikiri mnanipigia simu kunialiaka kwa harusi ya Wanjala, kumbe ni kupatanishwa?"

Wanjala hata hivyo ameshindwa kumweleza mpenzi wake wa zamani mbona anamuomba msamaha, Lucy ametaka kujua mbona Wanjala yuataka kusamehewa.

"Huwezi kuomba msamaha kama hujui kosa lako ni lipi?," amehoji Lucy .

Lucy pia amewaacha Gidi na Ghost na kicheko kwa maswali yake ya vituko na ucheshi walipotaka amwambie Wanjala kauli ya mwisho  ili wakenya wasikie, Aliwajibu;

"Mimi nilipendana na Wanjala sio wakenya, Kama wakenya wanataka kusikia nikisema hayo basi wangoje nifunge ndoa na wakenya".  Amesema Lucy ambaye jina lake la pili  ni Mapenzi. Kama hujafika pwani basi Lucy Mapenzi amewapa kionjo cha mambo. Kwa kumalizia tu,Lucy amesema bayana kwamba hamtaki Wanjala kumpigia simu tena .