Sababu za kumsimamisha Ali kazi baada ya kufichua ndege ya China

Kenya Airways wameeleza na kupeana sababu zao kwanini walimsimamsha kazi mfanyikazi Ali Gire kwa ajili ya video ambayo alituma katika mtandao wa kijamii ikionyesha jinsi ndege ya China Southern Airlines ilivyotua katika uwanja wa ndege wa JKIA.

Ali alisimamishwa kazi kwa kutuma video hiyo jumanne, ndege hiyo ilikuwa imewabeba abiria 239 kutoka nchina China.

Mnamo jana Ali Gire alisema kuwa anahofia maisha yake kwa sababu ya kitendo hicho na yamo hatarini.

Ni video iliosababisha wanchi kutoa hisia zao tofauti huku wakihofu kupata virusi vya Corona ambavyo vimesababisha vifo vya watu nchini China.

" Mnamo tarehe, 26 Februari KQ ilipokea barua kutoka kwa kampuni ya KAA, ikisema kuwa kumekuwa na video ambayo imesambaa katika mtandao wa kijamii

Na video hiyo imetikana na mmoja wa mfanyakazi wa KQ." KQ ilisema.

Kupitia taarifa jumapili mchukuzi wa taifa alisema kulingana na meneja wa rasilimali watu mfanyakazi huyo alisimamishwa kazi ili uchunguzi ufanyike na kufichua ukweli wa kitendo hicho.

"This process will be conducted expeditiously in a fair and transparent manner and in the meantime the employee remains on a full salary." KQ Ilisema.

Waliongeza na kusema kuwa wanaelewa kwanini wananchi wengi wamo tayari kujua ukweli kuhusiana na corona virus.

"We fully understand and appreciate the public interest generated by the suspension of our employees following the filming and circulation on social media of the arrival of china southern flights." Waliongea.

Ali ameshtakiwa kwa madai kuwa alikuwa anafanya kazi na kikundi cha magaidi kwa sababu ya jina lake Ali.

Jumamosikupitia kwa wakili wake, Danstan Omari alisema kuwa mteja wake alikuwa anataka kufungwa korokoroni kwa maana ana hofia maisha yake.

Ubalozi wa China ulisema kuwa abiria hao waliokuja na ndege hiyo walishauriwa wakae pekeyao kwa siku kumi na nne.