tuwei

Shirikisho la riadha nchini lafutilia mbali kambi ya mazoezi ya chipukizi wasiozidi miaka 20

NA NICKSON TOSI

Shirikisho la riadha nchini-AK limefutilia mbali kambi ya mazoezi ya wanariadha wa miaka wasiozidi  umri wa miaka 20 iliyokuwa imeratibiwa kuanza mwezi ujao.

Tangazo hili limejiri siku moja tu baada ya wizara ya michezo nchini kufutilia mbali mashindano ya wanariadha wasiozidi miaka 20 yaliyotarajiwa kuandaliwa Nairobi Julai kutokana na mkurupuko wa Corona.

Kamati andalizi ya mashindano hayo ilikuwa ishaanza kuweka maandalizi katika uwanja wa Kasarani ambapo mashindano yalikuwa yameratibiwa kufanyikia.

AK imesema kuwepo kwa virusi vya Corona nchini kumefanya wachukue hatua hiyo ili kuepusha maambukizi zaidi.

jackson tuwei

Tangazo hili linajiri siku chache tu baada ya kamati andalizi ya mashindano ya Olimpiki kuahirisha mashindano hayo hadi mwaka ujao mjini Tokyo, Japan mwaka huu.

 

Mhariri: Davis Ojiambo

Photo Credits: Radio Jambo

Read More:

Comments

comments