'Siamini hospitali," Hannah Khahugani apeana sababu za kuuweka mwili wa mwanawe

Mwalimu wa chuo kikuu cha Nairobi, Hannah Khahugani aliyetiwa mbaroni baada ya kupatikana na maiti ya mtoto wake nyumbani mwake South B hatimaye amezungumza.

Mwanamke huyo, sasa hivi amezuiliwa katika kituo cha polisi cha Industrial area.Mwanamke huyu jina lake Hannah Khahugani alikuwa mpangaji mpya wa ploti ya Kifaru.

Mtunza ploti wa Front Apartments, Stephen Mwangi aliripoti kifo cha mwanawe Khahugani, baada ya kwenda nyumbani mwake Hannah kuitisha kodi ya nyumba.

Na hapo ndipo aliposongea kwenye dirisha la chumba cha mapumziko na kuuona mwili wa Emmanuel sakafuni ukiwa umefunikwa na blanketi.

Kulingana na polisi, Khahugani alikuwa anaishi pamoja na marehemu mtoto wake kabla ya mtunza ploti hiyo kuwaarifu kuwa kuna harufu ya uvundo inayotoka kwenye nyumba yake.

Aliubisha mlango lakini hakuna aliyejibu. Hapo akampigia Hannah simu, aliskia simu ikilia kwa nyumba lakini hamna aliyejibu.

Hannah aliwaarifu polisi kuwa mwanawe alianguka na kuaga dunia. Alisema hakumpeleka hospitalini kwa sababu haamini hospitali. Mama huyo alisema kijana wake alianguka na kufariki ndani mwa nyumba yake iliyoko ghorofa ya sita.

“Alisema hakumpeleka hospitalini kwa sababu haamini mahospitali," Ndolo alisema.

HIki ni kinaya kwani Hannah amekuwa akiwapa mafunzi This is ironic because Hannah has been active in training wanaotoa huduma zaa afya.

Polisi wanaamini mwanamke huyo ni wa dhebu la kishetani. Sasa hivi amezuiliwa katika kituo cha polisi cha Industrial area akisubiri kufanyiwa tathmini ya hali yake ya akili.

Hili likifanyika litaamua kitakachofanyika na kesi hiyo.

Mwili wake Emmanuel ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti.