Sonko wa Redio Jambo awashtukiza wakaazi Meru. Amwaga hela kibao

Sonko wa kituo cha jambo hii leo ametua asubuhi na mapema mji wa Meru na kuwazawadi wasikilizaji kwa hela lukuki. Sonko huyu amewasili mji huo asubuhi na kuchana mjini kote kuwatafuta washindi wa The Phrase That Pays Redio Jambo Ongea Usikike.

Soma hapa:

Sonko amewazawadi Paddy Mwenda,Daniel Mugao,Martin Mutwiri na wengineo maelfu ya pesa. Wakaazi mjini meru wameonyesha tabasamu kubwa zaidi kwa kutembelewa na kituo hiki huku mapokezi yakiwa makubwa zaidi.

Tazama baadhi ya picha za washindi:

Sonko sasa anatarajiwa kutua kaunti ya Muranga hapo kesho na kugawa hela kwa mashabiki. Watu kutoka maeneo yanayozunguka miji kuu hapo kesho watafurahi zaidi kukutana na sonko kutoka redio inayoongoza nchini kwa matangazo na vipindi bora zaidi ya Jambo.Ikumbukwe kuwa zoezi hili linatarajiwa kuendeshwa hadi mwisho wa mwezi wa Agosti.