Usaliti:Twin sister yangu alitoroka na mume wangu’.Jennifer asimulia uchungu wa kusalitiwa

sad woman
sad woman
 Watu ambao huzaliwa kama pacha aghalabu huwa na uhusiano wa karibu  na kuanzia utotoni vitu vyao vingi hufanyika pamoja .

wazazi wa watoto pacha pia hujaribu kuwatengezea kila kitu kinachofanana ,na si ajabu wakati mwingi ukitembea barabara kuwaona watoto pacha wakiwa na nguo za mshono mmoja .Lakini kwa  Jennifer Nyokabi ,masaibu yaliyomkumba  baada ya dadake Peninah kutoroka na mume wake yamemfanya kutengana fikra kabisa na mtoto ambaye walizaliwa naye pamoja .Inakuaje kwamba damu ni nzito kuliko maji lakini mwanamme amewafanya dada pacha kukosana vibaya?

Jeni na Peni kama wanavyoitana kutoka utotoni walilelewa pamoja na kila jambo lao walilifanya pamoja  . Wamesomea Nyanyuki pamoja na hata kulelewa huko na wazazi wao.Kuanzia shule ya msingi hadi kila mtu alipojiunga na chuo kikuu wawili hao wamekuwa  pamoja .Baada ya kumaliza masomo ya vyuoni ,Jeni alipata kazi katika kampuni moja ya bima jijini Nairobi  na  alikokutana na mpenzi wake na baadaye wakafunga ndoa . Dadake  alikuwa nguzo muhimu sana wakati wa maandalizi ya sherehe ya harusi ya  Jeni  na hata ilifanywa kejeli kwamba Mume wake angefaa kuwachukua wote! Kumbe hawakujua yatakayowapata mbele .

Miaka miwili baadaye wakati Peni alipokuja Nairobi alikopata kazi ,wawili hao walirejelea uhusiano wao wa kuwa karibu na hata  dada hao wakajipata wanaishi katika mtaa mmoja karibu na kila mwenzao. Peni na Jeni walionekana pamoja kila wakati isipokuwa walipoelekea kazini .John ,mume wa Jeni pia alianza uhusiano wa karibu na shemeji yake lakini hakuna aliyeshuku lolote .

Iilipasulia mbarika mwaka wa 2018 wakati Jeni alipompata mumewe amepakia nguzo zake zote akisema ameamua kuondoka kutoka nyumba ili kutuliza fikra kwa sababu ya malumbano ambayo yalikuwa yameanza kushirika kasi katika ndoa yao .Alichokosa kujua Jeni ni kwamba John ,alikuwa akielekea kuishi na dadake pacha Peni! Yalimfika kama  radi na hakuweza kufahamu  mume wake na dadake walianza uhusiano wa kimapenzi lini na hata kabla ya yeye kuweza kupata majibu  ,Peni na John walihamia Mombasa kuanza upya maisha yao . Peni alikuwa akifanya kazi na  wizara  afya na kwa sababu ya ugatuzi alipata uhamisho wa kwenda Mombasa ndiposa akaamua kwenda na mume wa dadake . Jeni alipatwa na mshtuko ambao uliathiri utendkazi wake kazini na hata fikra zake zikasumbuka asiweze uendelea na maisha .Amepata usaidizi kwa kujiunga na kundi la waathiriwa waliopitia mambo yaliyotikisa maisha yao na wanaohitaji msaada wa ushauri  na katika kundi lao ,wanasaidiiana ili kuweza kustahimili machungu wanayopitia.

Unafikiri Jeni anafaa kumlaumu nani? Dadake au mume wake?