Deadbeat: Nilipata mimba akanitoroka na kuniita mwendawazimu

Muhtasari

• Ann,21, anasema mwanamme aliyepata na yeye mtoto alikataa kushughulikia malezi na kumuita mwendawazimu na mjinga.

• Alipopata mimba yake, jamaa alimtoka akamtelekeza na kutorokea Nairobi.

Massawe Japanni
Image: INSTAGRAM

Ann,21, anasema mwanamme aliyepata na yeye mtoto alikataa kushughulikia malezi na kumuita mwendawazimu na mjinga.

Mwanamme huyo, 33, waliyepatana katika chuo anuwai ambapo walikuwa wanasoma Pamoja na alipopata mimba yake, jamaa alimtoka akamtelekeza na kutorokea Nairobi.

“Nilipomwambia niko na mimba yake aliniruka na akamaliza masomo na kukimbilia Nairobi. Kumpigia simu akapatia wasichana wakaanza kunitusi,” alisema Ann

Ann anaeleza kwamba aliacha kumpigia simu kwa sababu alisikia vibaya kutukanwa na akaona akiendelea kuongea na yeye atakasirika na pengine kupata majaribu ya kutoa mimba hiyo. Aliamua kuilea mimba na baadae akazaa mtoto njiti.

Alishinda hospitalini na mtoto wake akilelewa kwa msaada wa oksijeni katika kiangulio na baadae akaruhusiwa kuelekea nyumbani na mwanawe.

“Kuenda nyumbani tulikaa na mama yangu na nikampigia nikamtaarifu nimejifungua mtoto. Nilimtaka anisaidie kushughulikia mtoto wake lakini yeye alianza kunitusi kwamba mimi ni mjinga na mwenzawazimu,” alielezea.

Baadae mamake Ann aliwatafuta wazazi wa mwanamme huyo na pamoja wakaongea na kuelewana na huyo mwanamme kwa simu kwamba atakuwa anashughulikia mwanae.

Baadae mwanamme huyo aliporudi nyumbani mamake alimwambia atii ahadi yake ya kushugjhilia mtoto wake lakini jamaa aliruka hiyo stori na kusema kwamba hata hamjui Ann.

“Juzi nimempigia nikamwambia kama hawezi shughulikia mtoto wake nitamripoti kwenye ofisi za kushughulika maslahi ya watoto, yeye alianiambia ninaweza mripoti popote na simtishi,” Ann alielezea Massawe.

Massawe alipompigia simu mwanamme huyo alikuwa azazungumza kwa ukali bila kutaka kusikia chochote kuhusu mtoto wake, jambo lililopelekea Massawe kumuahidi Ann kushirikiana na yeye na kumripoti huyo jamaa ili ashrutishwe kushughulika malezi ya mwanae.