Watu hawakujua nilipopatwa na corona wajukuu na wafanyakazi wangu 7 walipatwa na corona-Margaret Wanjiru

Muhtasari
  • Askofu Margaret Wanjiru afichua kuwa wajukuu wake na wafanyakazi wake 7 walipatwa na corona
Askofu Margaret Wanjiru
Image: Studio

Kaika kitengo cha ilikuaje tulikuwa naye askofu Margaret Wanjiru, ambaye ameweka wazi kwamba atawania kiti cha ugavana katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

Maragaret aliuma sana mwaka jana baada ya kupatikana na virusi vua corona, huku akizungumzia suala hilo alisema kuwa;

"Niliposikia dalili nilienda hospitali lakini niliambiwa kuwa naugua kwa sababu nilikula chakula ambacho kilikuwa na sumu

Baada ya siku kadhaa daktari aliniambia kwamba napswa kupimwa corona, na nikapatikana nayo, nilipelekwa ICU siku chache baada ya kulazwa kwa sababu nilikuwa na shida ya kupumua

Nilikaa huko kwa siku tatu, ambapo baada ya kutibiwa daktari aliniambia kwamba sina corona,nilipata nguvvu nikamwambia anipe ruhusa niende nyumbani

Sababu yangu kuu ya kufichua kwamba nilikuwa na corona, nilitaka maombi, watu wengi walikuwa wanaogopa unyanyapaa ukificha shida yako utaombewa aje nilikuwa nataka maombi kutoka kwa wananchi

Kile amabcho watu hawakujua ni kuwa wajukuu wangu pia walilazwa hospitali kwa ajili ya corona, pamoja na wafanyakazi wangu 7

Nilikuwa nimeambia Mungu kama mbingu iko tayari kunipokea ata mimi niko tayari, lakini cha muhimu niliambia Mungu akinipa nafasi ya pili nitatumikia watu wake, pia nilikuwa najiuliza nitaacha urithi upi baada yangu ya kuaga dunia," Alizungumza Margaret.

Huku akijipigia debe alisema kwamba atabadili mji wa Nairobi uwe msafi kwani kuna uchafu mwingi.

"Nairobi ina uchafu mwingi na ajenda yangu ya kwanza ni kusafisha Nairobi na kuleta mabadiliko makubwa kama maji, yatakuwa hakutakuwa na trafiki itakuwa Nairobi mpya

Sababu yangu ya kusimama na naibu rais William Ruto, ni kwa ajili  amesimama na maono yangu ya kuendeleza mji wa Nairobi

Nitaendelea kuwa Askofu na ata uwa gavana wa Nairobi, kwani awali nimekuwa nikifanya siasa na kuwa askofu

Biblia inasema mtakatifu akitawala mji utafurahi, kwa hivyo mji wa Nairobi utafurahi."

Kwa mengi zaidi tebelea Radiojambo Youtube.