Patanisho: Jamaa atorokea Mombasa baada ya kumpa mimba mwanafunzi wa darasa la 8

Muhtasari

•Celestine alisema kuwa ndoa yake ya miaka saba ilisambaratika mnamo Februari mwaka jana kufuatia tabia za mumewe za kukanyaga  nje ya ndoa.

•Alifichua kuwa mumewe alipokuwa Mombasa aliacha kama amepachika msichana mwingine ujauzito.

Gidi na Ghost
Gidi na Ghost
Image: RADIO JAMBO

Katika kipindi chetu cha Gidi na Ghost asubuhi kitengo cha Patanisho, mwanadada aliyejitambulisha kama Celestine (23) alituma ujumbe akiomba kupatishwa na mumewe Isaac (27).

Celestine alisema kuwa ndoa yake ya miaka saba ilisambaratika mnamo Februari mwaka jana kufuatia tabia za mumewe za kukanyaga  nje ya ndoa.

"Alikuwa mhanyaji. Alikuwa mtu wa wanawake sana juu alikuwa mtu wa boda. Alikuwa anatoka kazini kisha akifika kwa nyumba anaanza kunichapa. Nikiuuliza sababu za kunichapa alikuwa ananiambia kuwa hanitaki kwa hiyo nyumba. Nilimuuliza mbona hanitaki na tayari tumezaa naye watoto. Nakamwambia angeniambia mapema ili nijipange," Celestine alisimulia.

Celestine alifichua kuwa mumewe alianza tabia ya kuenda nje ya ndoa na katika harakati hizo akampachika ujauzito msichana wa darasa la nane.

"Wazazi wa msichana huyo walimleta ili aweze kumlea. Akatoroka msichana huyo akaenda Mombasa. Alimaliza mwaka mmoja Mombasa mimi nikabaki tu kwa boma. Aliporudi aliniuliza mbona bado sijatoka, akanichapa akanitoa damu," Alisema.

Mwanadada huyo alifichua kuwa mumewe alipokuwa Mombasa aliacha kama amepachika msichana mwingine ujauzito. Kama kesi ya kwanza tu, wazazi wa msichana huyo pia walimkabidhi binti yao ili amshughulikie.

Alisema kuwa kwa sasa mumewe anaishi Nairobi na watoto wao wawili. Alieleza wasiwasi wake kuwa watoto wake wanateswa pale na Isaac amekataa nao.

 "Nataka kujua msimamo wake. Kama atakubali nirudi ni sawa, kama atakataa ni sawa," Alisema.

Juhudi za kumfikia Isaac ili kumpatanisha na Celestine hata hivyo ziliangulia patupu kwani alikuwa amezima simu yake.

Je, una ushauri upikwa Celestine?