KITENGO CHA PATANISHO

Mwanaume alia kuachwa na mkewe kwa sababu ya matope

Niliingia nyumbani kiatu kikiwa na matope halafu kesho yake akatoka akaniacha

Muhtasari

•Nilikuwa nimetoka matanga, nikaruka mto nikafika nyumbani kiatu kikiwa na matope, halafu naye bibi yangu akasema naye pia anatoka aende matanga kwao, hata sikumfukuza.

•Unafikiria nini juu unipeleke Radio Jambo? Sitaki kusikia mambo yakr ananipigia tu kelele. Mwuulize nilimkosea kosa gani ili anilete huko.  Mwambie basi atume fare saa hii saa hii.

GHOST NA GIDI STUDIONI
GHOST NA GIDI STUDIONI GHOST NA GIDI STUDIONI
Image: RADIO JAMBO

Katika kitengo cha patanisho, Vincent Sony ameomba kunusuriwa ndoa yake baada ya mkewe Sandra Mwenesi kumtelekeza alipougua Mei 20.

Katika mawasiliano na Radio Jambo, Vincent ameeleza kwamba mkewe alimtoroka alipofika nyumbani huku viatu vyake vina matope na nguo zake kulowa maji akamshuku labda alikuwa na mwanamke mwingine.

“Nilikuwa nimetoka matanga, nikaruka mto nikafika nyumbani kiatu kikiwa na matope, halafu naye bibi yangu akasema naye pia anatoka aende matanga kwao, hata sikumfukuza.Alikuja na mtoto lakini nilikuwa namshughulikia kama wangu, hata alikuwa anakunywa soda kubwa kila wiki. ” Alieleza Vincent.

Kulingana na Sndra, 21, ameeleza kwamba yeye hataki maneno ya Vincent na iwapo anamtaka aweze kumtunmia nauli papo hapo.“Unafikiria nini juu unipeleke Radio Jambo? Sitaki kusikia mambo yakr ananipigia tu kelele. Mwuulize nilimkosea kosa gani ili anilete huko.  Mwambie basi atume fare saa hii saa hii. Mimi sitaki watu huku, maneno yake nimekataa. ”

Mawasiliano na juhudi za kuwapatisha wawili hao ziligonga mwamba, ambapo mpenziwe Vincent alikatisha mawasiliano hayo na kueleza kwamba masiliano ya mumewe hataki.

Vincent alikiri kwamba alimpenda mkewe na kama ingewezekana arejee nyumbani angefurahi sana. Kwa kuzidikana kwa mawasiliano hayo, kulimuacha Vincent kuomba kutafutiwa mke wingine.“Kama amekaatako mnaweza nitafutieko mwingine huko radio jambo?” Alisihi.