KITENGO CHA PATANISHO

Patanisho: Jamaa alia kuachwa baada ya kubagua mtoto wa mkewe

Huyo mwanaume anabagua watoto, anapenda wake lakini wangu hampendi, akuje aulizwe swali na shosho ajibu - Nyambura

Muhtasari

•Shida yake ni kutaka niwe pamoja naye kila wakati na kama mwanaume inafaa nipitepite kidogo ili nitulize akili.

Image: RADIO JAMBO

PATANISHO: Katika kitengo cha patanisho, Daniel Ng’ang’a ameomba kupatanishwa na mkewe Grace Nyambura, waliokaa katika ndoa kwa miaka 3.

Ng’ang’a amekiri kuwa walikosana na mkewe kutokana na mzozo wa nyumbani kati yake na mkewe, kilichochangia kumchapa ingawa hata baada ya hiyo waliutatua mzozo ingawa aliporejea nyumbani kutoka kazini alimkuta mkewe ameondoka na watoto.

Naomba mnipatanishe na wife yangu Grace Nyambura, tumekuwa naye katika ndoa kwa miaka mitatu. Tulikosana naye na akaenda kwao. Tuligombana naye kwa nyumba halafu nikamchapa.

Alikasirika lakini tuliongea mambo ikaisha, halafu akaanza kunishuku kuwa nina mpango wa kando. Niliporudi nyumbani nilimkuta ameondoka,” Alisimulia Ng’ang’a.

Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 26 alieleza kuwa tatizo kuu lilikuwa mkewe kumchunguza sana huku akieleza kuwa alitaka wawe naye pamoja kutoka kazini na kurejea nyumbani kama walivyoenda huko pamoja, jambo ambalo Ng’ang’a alisema kuwa alihitaji muda kidogo wa kujituliza akili.

Kama mwanaume, inafaa nipitepite kidogo nitulize akili. Yeye anataka tu, tukienda kazini anataka turudi nyumbani pamoja, na mimi nilikataa hilo,” Aliendelea.

Kwa upande wake Nyambura, alieleza kuwa mzozo uliibuka kutokana na mumewe kuwabagua watoto. Alimpenda mwanawe waliopata pamoja na Nyambura ila alimchukia sana yule mkewe aliyekuja naye kwenye ndoa.

“Mimi si mama wa mtoto, mmoja, nina watoto na siwezi tupa mtoto mmoja juu ya mwanaume, heri nikae hivyo bila mwanaume ,,yeye anabagua watoto,,aliniambia kama natoka kwake, nichukue mtoto wangu niache wake, nikaona kuliko iendelee sana nijitoe, issue ya huyo mtoto ni moja tu, hamuiti dad,” alisema Nyambura

Mwadada huyo huyo alieleza kuwa ari ya bwanake kutaka warudiane kwa kupatanishwa na wazazi wao, haitafua dafu kwani alikiri kuwa yeye amelelwa na nyanya yake na wala si mamake kama Ng’ang’a anavyodai.

Usiniulize maswali mimi. Fuata vile uliambiwa, fullstop. Mimi sina stori nyingi. Wazazi wangu wako hai lakini si hao walinilea. Nimekwambia uje kwa shosho, shosho ndiye anajua shida zangu. Ukuje kwa shosho yangu,” Aliendelea.

Ungetoa ushauri gani kwa Daniel?