Patanisho: "Wewe achana na bibi yangu, watoto wangu!" Jamaa aonywa na nduguye mkubwa

"Mimi sina ubaya. Kama ni matusi uache. Nimekuacha na miaka 10, sasa unanitusi matusi chafu hadi nashindwa kuelewa," Wilfred alimwambia nduguye.

Muhtasari

•Gilbert alisema uhusiano wake na nduguye uliharibika walipokorofishana baada ya baba yao kuuza shamba.

•"Alikuwa anatupa maneno chafu nashindwa mke wangu hajamkosea. Lakini ni sawa tu. Namsamehe huyo jamaa," Wilfred alisema.

Ghost na Gidi
Ghost na Gidi
Image: RADIO JAMBO

Gilbert Morang'a ,23, alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na  ndugu yake mkubwa Wilfred Morang'a ,33, ambaye alikosana naye mwaka jana.

Gilbert alisema uhusiano wake na nduguye uliharibika walipokorofishana baada ya baba yao kuuza shamba.

"Mzee aliuza shamba kipande kidogo. Alijenga nyumba yake na mimi akanijengea yangu. Mimi nilikuwa nataka nipewe pesa zote,"  Gilbert alisema.

Aliongeza, "Nilitusi ndugu yangu na mke wake. Nimejifikiria vizuri nikaona mimi ndiye mwenye makosa. Kwa sasa siwezi kuongea na yeye vizuri, tukiongea tunakosana tu. Ile utoto nilikuwa nayo nimeacha."

Bw Wilfred alipopigiwa simu, Gilbert alichukua fursa hiyo kumuomba msamaha kwa maovu yote ambayo alimfanyia.

"Naomba unisamehe kwa kukutusi na kutusi bibi yako. Nimeongea na watu wengu nikaambiwa mimi ndiye niko na shida," alisema Gilbert.

Wilfred alimwambia, "Mimi sina ubaya. Kama ni matusi uache. Nimekuacha na miaka 10, sasa unanitusi matusi chafu hadi nashindwa kuelewa."

Gilbert alikiri kufurahishwa na msamaha wa kakake na kubainisha kuwa sasa ataweza kumtembelea bila wasiwasi.

"Sasa hadi nimekuwa free, ata roho yangu imefunguka.  Naomba anitoe blacklist nimpigie simu sasa hivi," Gilbert alisema.

Wilfred alifunguka kuhusu masaibu ambayo kaka huyo wake mdogo alimpitishia hadi kufikia hatua ya kumblock.

"Wakati mwingine hata nilikuwa nazima simu nashindwa bro ananitusi kwa nini. Nikiangalia naona sijakosea, hata bibi hatugawani. Vita sio ya maana. Nilikuwa namwambia kama ni kitu anataka aseme. Mimi ata nilikuwa namsomesha kidogo akaachia darasa la nane sijui ni kazi gani anafanya. Alikuwa anatupa maneno chafu nashindwa mke wangu hajamkosea. Lakini ni sawa tu. Namsamehe huyo jamaa," alisema.

Gilbert alimshukuru ndugu huyo  wake kwa kumsamehe na kubainisha kuwa sasa wataishi kama mandugu.

Wilfred alimwambia, "Mimi sina ubaya na wewe. Niliambia hadi chifu nyumbani. Wakanimbia niachane na wewe.Wewe wachana na bibi yangu, wachana na watoto wangu. Tuishi kama ndugu. Watoto wangu ni wako, na watoto wako ni wangu. Kumbuka mahali nimekutoa.