Wagonjwa walio na virusi vya ukimwi wagadhabishwa

Dawa zinazotumika kupunguza makali ya virusi vya ukimwi mwilini ARV, kwa sasa zitakuwa zinagawanywa kwa kutumia makontena makubwa kama ilivyotangazwa na PEPFAR (President's Emergency Plan For Aids Relief) kampuni inayofadhili tembe hizo.

Tukio ambalo limewagadhabisha watu wanaougua virusi hivyo wakisema kuwa litasababisha hali ya unyanyapaa.

Kampuni hiyo imesema kuwa hatua hiyo itapunguza gharama ya kusambaza dawa hizo kutoka shillingi billioni 50.5 chini mpaka billioni 35, huku wakitaka wizara ya afya kutayarisha makontena makubwa ambayo inaweza beba tembe 100-180.

Aidha kampuni hiyo imeongeza kuwa wanaougua ugonjwa huo watakuwa wanatembelea kituo cha afya mara moja kwa miezi tatu ama hata miezi sita.

Mwenyekiti wa kundi ya kushawishi wanaoishi na virusi hiyo Nelson Otuoma, amesema kuwa hatua hiyo ni wazo mbaya kwani watu wanaougua ugonjwa huo hawajakaribisha hatua hiyo manake wanapendelea dawa hizo zikiwa kwa makontena madogo.

Mashirika ya tiba nchini pia yameonekana kupinga wazo hilo wakisema kuwa wagonjwa wengi wanapendelea kutembelea kituo cha afya kila mwezi na hawana shida hata wakipewa makontena ndogo kadhaa ya tembe hizo.

Kulingana na takwimu iliyofanyika hivi majuzi, karibu watu millioni 1.5 nchini Kenya wanaishi na virusi hiyo, huku watu millioni moja wakitumia tembe hizo za ARV's inayogharimu shillingi billioni 20, asilimia 20% ikifadhiliwa na serikali ya Kenya, huku kampuni ya PEPFAR (President's Emergency Plan For Aids Releif) ikifadhili asilimia 80%