Wema Sepetu alaumu Kanumba kwa shida zake za uzazi

wema sepetu
wema sepetu
Mrembo Wema Sepetu ambaye aliwahi shikilia taji la 'Miss Tanzania' amemlaumu aliyekuwa mpenzi wake na aliyekuwa muigiaji, hayati Kanumba kwa shida zake za kutopata watoto.

Wawili hao walikuwa kwenye uhisiano ambao ulifeli.

Akizungumza katika mahojiano wa moja kwa moja kupitia 'Wema App' kidosho huyo alifunguka na kusema kuwa akiwa kwenye uhusiano huo, aliavya mimba mara mbili.

Mimba ya kwanza alisema kuwa aliavya baada yake na Kanumba kukubaliana, huku akiongeza kuwa aliavya mimba ya pili bila ya Kanumba kujua.

Kulingana na mpenzi huyu wa zamani wa Diamond Platnumz, sababu ya kuavya mimba hizo mbili ni eti Wema alihisi kuwa alikuwa mchanga sana kupata watoto wakti huo.

“I feel like Kanumba cursed me. This is because he wanted to see me, he would call every day two weeks before his death,” alisema.

"We were to meet but we were super busy and could not. He called for like four times but we could not meet. We finally met at Bilcanas."