Wosia wa Jackson Kibor kwenye Kongamano la Wanaume Eldoret

Kibor-compressed
Kibor-compressed
Kongamano la kwanza la wanaume lilifanyika Jumatatu katika mji wa Eldoret huku  mzee Jackson  kibor akitoa wosia zake za busara kwa wanaume kuhusu ndoa na uadlifu.

Kibor aliwasihi wanaume wawe watulivu, dhabiti na kuepuka kuhadaiwa na wanawake.

Kauli mbiu ya Kongamano hilo ni ''Wanaume na  Milima Saba ya Ushawishi wa Kijamii."

Mzee huyo mwenye umri wa miaka 85, alisema kwamba siri kuu ya kuwa na maisha marefu ni lishe bora na kuthamini vyakula vya asili.

Katika kongamano hilo la kipekee lilihudhuriwa na mamia ya wanaume, Kibor aliwatahadharisha wanaume dhidi ya kuzembea na kutegemea wazazi wako kwa kila jambo.

Kibor pia aliwarai vijana kuepuka ndoa ya dhuluma na mateso kabla ya ndoa hiyo igeuke kuwa janga la mauti.

Mzee huyu anayefahamika sana kutokana na ukulima wa mahindi katika eneo la Uasin Gishu alisimama jukwaani huku wanaume wote ukumbuni wakimpa masikio kutokana na uweledi wake kwenye masula ya ndoa.

Kibor aliwasihi wanaume kuwa waja  Mungu kwa kuwa ni yeye tu ajuaye maisha ya binadamu.

"Jambo la kwanza ni kumheshimu Mungu, hakuna mtu ajuaye Mungu yuko wapi" Kibor alisema.

"Mtu aliyeanzisha starehe ni nani ?" Kibor aliuliza.

Mwishowe Kibor aliwamotisha wanaume kutokata tamaa."Usikate tamaa, tia bidii na Mungu atakufungulia njia"

alisema.