Yoweri Museveni ataja hali ya ukata aliokulia Eddy Kenzo, ampongeza

EH_1jZuX4AEudLz__1572352901_37362
EH_1jZuX4AEudLz__1572352901_37362
Staa na nyota wa Uganda Eddy Kenzo amepata nafasi ya kupatana na rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni.

Tofauti na kuwa Eddy anafanya freshi kimuziki, staa huyu amekuwa katika mstari wa kwanza kumkosoa Museveni.

Yoweri alikuwa amemuita Kenzo katika ikulu ili kumpa kongole za kutwaa ushindi AEA-USA.

Tuzo hizi ziliandaliwa nchini Marekani.

Muimbaji huyu alikuwa akiteta kuhusu kisa na ambapo Sheikh Nuhu alitoa matamshi ya chuki mbele ya binti yake.

Kulingana na Kenzo, Nuhu alimshushia hadhi sana.

Kufikia sasa hakuna hatua imechukuliwa dhidi ya muhubiri huyu.

"Nilikutana na nyota aliyetawazwa mtumbuizaji bora Afrika na mshindi wa BET, Edrisah Musuuza almaarufu kama @eddykenzoficial. Hadithi yake ni ya kujikakamua na kazi kubwa..." Alichapisha Museveni.

https://twitter.com/KagutaMuseveni/status/1188868569792155648

Kiongozi huyu wa dini alitoa cheche za matusi kuwa Kenzo ni maskini, anayechepuka na hangeweza kuoa Rema.

https://twitter.com/eddykenzoficial/status/1188894236994932736

"Nashukuru kwa kauli zako za kunipa moyo...Nitangaze kuwa tulipatana na rais Entebbe..." ilisoma tweet ya Kenzo.

Kenzo aliweza kutokwa na machozi baada ya cheche hizo kutokea.