12 Wafariki huku visa vya covid19 vikifika 10,294

Kenya  leo imesajili  idadi ya juu ya watu walioaga dunia kwa siku moja kutokana na ugonjwa wa corona baada ya watu 12 kuaga dunia.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe amesema wote walioaga dunia ni kutoka Nairobi. Amesema watatu waliaga dunia wakiwa nyumbani ilhali waliosalia walifariki wakiwa hospitalini.

Kagwe ameongeza kwamba visa 189 vya ugonjwa huo vimeripotiwa nchini katika saa 24 zilizopita na kufikisha jumla ya visa hivyo nchini kuwa  10,294.

Visa hivyo ni kutoka kwa sampuli 1,205  na kufikisha jumla ya sampuli zilizopimwa hadi sasa kuwa  216,242.

Kati ya visa hivyo vipya, 106 ni  vya wanaume ilhali 83 ni wanawake .

Nairobi inaendelea kaunti inayoongoza kwa idadi ya visa vingi baada ya watu 147 kupatikana na virusi hivyo. Kaunti nyingine ni

Kiambu 20, Machakos 11, Kajiado 5  na Mombasa 2.

Waziri Kagwe amesema sampuli nyingine zilizokusanywa leo hazijapimwa kwa sababu ya changamoto ya kielektroniki .