OPARESHENI ya siku 11 ya kuisaka miili ya mama na mwanawe waliozama katika bahari hindi huenda ikazaa matunda leo usiku au kesho asubuhi baada ya wapiga mbizi kuona mabaki ya gari walilokuwa ndani .msemaji wa serikali Cyrus Oguna amesema kifaa hicho kimegunduliwa kimo cha mita 58 chini ya bahari.
Bunge la kaunti ya laikipia limekuwa la 12 kuukata mswada wa punguza mizigo . waakilishi wa kaunti hiyo wamesema mswada huo wa muungano wa thirdaway alliance haujaafikiwa vigezo kadhaa ikiwemo kutohusishwa kwa wananchi kabla ya kuwasilishwa katika bunge hilo.
Huku hayoa yakiarifiwa kiongozi wa thirdawya alliance Ekuru Aukot amewashtumu wanasiasa kwa kujaribu kusambaratisha juhudi za kuupitisha mswada wa punguza mizigo licha ya mswada huo kuendelea kukataliwa na mabunge ya kaunti . Aukot amesema wanasiasa wanawatumia wakenya na waakilishi wa kaunti kuukata mswada huo ili kulinda maslahi yao .
Iwapo unapanga kumtembelea rafiki au jamaa hapo kesho ,angalau hakikisha umabeba zawadi ya kumpa.mwanasosholjia Kennedy Ong’aro anasema kumzuru mtu ukiwa mikono mitupu au na zawadi ya gmara ya chini ni jambo la kufedhehesha hasa iwapo hamjaonana kwa muda mrefu .
Mwanamme mmoja nahofiwa kuaga dunia baada ya shimo la choo alililokuwa akichimba kuporomoka na kumfunika katika kijiji cha marobo huko bungoma . shimo hilo la choo katika shule moja ya upili lilikuwa limefika kimo cha futi 25 .
Kando na wafanyikazi katika sekta ya kibinafsi ,watumishi wa umma pia wapo katika hatari ya kupoteza kazi zai kwani serikali ina mpango wa kupunguza idadi ya wafanyikazi wake katika siku chache zijazo . mtaalam wa masuala ya uchumi Charles karisa amesema kampuni nyingi zinafungwa au kuwafuta kazi wafanyikazi kwa sababu ya gharama ya juu ya leba na oparesheni hatua ambayo itaathiri pato la jumla la nchi .
Gavana wa machakos Alfred Mutua anataka waranti ya kuka,atwa kwake iliyotolewa kwa kukaidi kufika mbele ya kamati moja ya senate kufutuliwa mbali . MuTUA ALIKATAA Kufika mbele ya kamati ya senate kuhusu UHASIBU mara mbili akisema mazingira ya vikao hivyo hayakuwa salama .
Spika wa Nairobi Beatrice Elachi amesalia afisini mwake licha ya kundi moja la waakilishi wa kaunti wanaompinga kujaribu kumfurusha .elachi amemlaumu kiongozi wa walio wengi katika bung la kaunti Abdi Guyo kwa masaibu yake .
Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu wamewalaumu polisi kwa kutumia nguvu kupita kiasi wakati wa kuwakabili washukiwa waliomwua afisa mmja wa polisi ambaye mwili wake ulipatikana siku ya jumamosi .Hussein Khalid kutoka haki Africa badala yake amewarai polisi kutumia njia mbadala za kupata habari kutoka kwa wananchi na sio kuwanyanyasa .
Wahudumu wa matatu kutoka mlima Kenya wametishia kulemaza huduma za usafiri ili kulalamikia agizo la kuwataka waweke vidhibiti mwndo vipya katika magari yao .wamesema agizo hilo la NTSA linawatwika mzigo wa gharama zaidi kwani hawakushauriana na NTSA kuhusu uamuzi huo wala kueleza kasoro za vidhibiti mwendo wanavyotumia sasa .
Polisi huko eldoret wamewakamata washukiwa watano wa wizi wa mifugo na kupata mifugo waliobwa kutoka west pokot .kamanda wa polisi katika kaunti hiyo johnstone ipara amesema washukiwa hao ni pamoja na afisa mmoja wa zamani wa KDF ilhali washukiwa watatu walitoroka .
Maafisa wa polisi nchini Uganda wamefutilia mbali tamasha la mbunge wa Kyadondo mashariki Robert Kyagulani maarufu Bobi Wine lililotarajiwa kufanyika karibu na mji mkuu wa Kampala.Naibu inspekta jenerali wa polisi Asuman Mugyenyi anasema kwamba waandalizi wa tamasha hilo walishindwa kuweka usalama uliohitajika, kulingana na chombo cha habari cha Nile Post.