Rais Uhuru Kenyatta ametuma ujumbe wa kumpongeza waziri mkuu wa Ethiopia Ahmed Abiy kwa kushinda tuzo ya amani ya Nobem mwaka huu . Abiy ametangazwa mshindi wa tuzo hiyo hivi leo kwa ajili ya juhudi zake kuleta maafikiano kati ya nchi yake na Eritrea ambazo zimekuwa zikizozana kuhusu mpaka kwa miaka 20.
Katika saa 17 zijazo mwanariadha bora wa mbio za marathon Eliuv Kipchoge atafanya jaribio la kihistoria la kukimbia mbizo za kilomita 42 chini ya saa mbili ili kudhihirisha kwamba binadamu anaweza kuafikia lolote bila vikwazo . mshikilizi huyo wa rekodi ya dunia anataka kuweka rekodi mpya ya saa moja na sekunde 59 katika mbio za INEOS 159 hapo kesho huko vienna Austria .
MAHAKAMA Kuu imefutilia mbali waranti ya kukamatwa kwa gavana wa machakos Alfred Mutua ikisema inakiuka haki zake za kikatiba . korti pia imemzuia inspekta mkuu wa polisi dhidi ya kuchukua hatua kuhusiana na waranti hiyo hadi kesi hiyo isikizwe na kuamuliwa .
Rais Uhuru Kenyatta amepongeza makundi ya uokoaji wa dharura yaliyoko katika Uwanja wa Ndege wa Wilson, Jijini Nairobi, kwa kuchukua hatua za haraka kufuatia ajali iliyohusisha ndege ya shirika la Silverstone aina ya Fokker 50.Wakati huo huo, Rais amewatakia uponyaji wa haraka waliojeruhiwa katika ajali hiyo ya ndege.
Iwapo kuna binadamu anayeweza kuvunja rekodi ya saa mbili ya mbio za marathon ,basi ni Eliud Kipchoge . Hii ndio kauli ya waziri wa michezi Amina Mohamed ambaye anampigia upatu Kipchoge kuivunja rekodi hiyo hapo kesho endapo kila hali itakuwa nzuri .
Chuo kikuu cha Moi kimefungwa kwa muda usiojulikana baada ya wanafunzi kuzua rabsha wakilalamikia usimamizi mbaya . wanafunzi wamehamakishwa na kuongezwa kwa ada ya mtihani wa ziada na kanuni mpya kuhusu matumizi ya vyumba wanavyotumia kulala . ada ya mtihani wa ziada imezidishwa hadi shilingi 1000 kutoka shilingi 400.
Sarah Wairimu, ,mjane wa raia wa udachi marehemu Tob Cohen ameachiliwa huru kwa dhamana . sarah ambaye ndiye mshukiwa mkuu katika mauaji ya mumewe ameachiliwa na mahakama kwa dhamana ya shilingi milioni 2 pesa taslimu .hata hivyo jaji Stella Mutuku ameamuru kwamba sarah hafai kukaribia majengo ya biashara za marehemu Cohen .
Kaunti ya taita taveta imeanza kuwahesabu wafanyikazi wake katika jitihada za kuwaondoa wafanyikazi feki na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi . mkurugenzi wa mawasiliano wa kaunti hiyo Dennis Onsarigo amesema wakati wa shughuli hiyo ya siku mbili wafanyikazi wote watahitajika kuripoti katika afisi za kaunti ndogo na yeti vyao vya masomo pamoja na barua za uteuzi .
Huku hayo yakiarifiwa Notisi ya kuondolewa afisini kwa gavana wa kaunti ya Taita Taveta Granton Samboja sasa imewasilishwa kwa spika wa seneti Ken Lusaka.Waakilishi wa wadi waliwasilisha notisi hiyo mapema hii leo huku Lusaka sasa akitarajiwa kuanza mchakato wa kuchunguza madai yaliyoibuliwa katika hoja ya kumbandua Samboja Katika kipindi cha siku saba kwa mujibu ya sheria Kama anavyoeleza mwenyekiti wa kamati ya bajeti GODWIN KILELE.
Bunge la Kaunti ya Trans Nzoia leo limewaalika wananchi kutoa maoni yao kuhusu mswada wa punguza mizigo .matokeo ya mchango huo wa wananchi yataamua iwapo waakilishi wa kaunti hiyo wataupitisha au kuukata mswada huo uliopendekezwa na muungano wa Thirdway Alliance .
Oparesheni ya kuiondoa miili ya mama na mwanawe waliotumbukia katika bahari hindi huko likoni inaendelea huku serikali ikiwa na matumaini ya kumaliza shughuli hiyo hivi leo . msemaji wa serikali Cyrus Oguna amewarai wakenya kuwa na subira kwani wanafnya kila wawezalo kuiondoa miili hiyo ,baada ya siku 13 .
Huku ulimwengu ukiadhimisha siku ya mtoto wa kike leo ,wahadhiri wa kike kutoka chuo kikuu cha kibabii wametoa msaada wa vitambaa vya hedhi ya wasichana wa shule huko bungoma .wakiongozwa na Caroline Namunan ,WAHADHIRI hao wamesema wasichana wa shule hasa katika maeneo ya mashambani hupitia changamoto kubwa kwa ajili ya ukosefi wa vitambaa hivyo na baadhi yao hukosa kwenda shule wakati wanapopata hedhi .
Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed ameshinda tuzo ya mwaka huu ya amani ya Nobel . kamati ya tuzo hiyo kutoka Norway imetoa tangazo hilo la kumpa Abiy taadhima hiyo kwa ajili ya juhudi zake za kuleta amani kati ya Ethiopia na taifa jirani la Eritrea kwa ajili ya mzozo wa muda mrefu wa mpakani . Ahmed alitajwa kuwa mshindi wa 100 wa Nobel Peace Prize huko Oslo.