Mambo 8 kuhusu Fibroids ambayo kama mwanamke unafaa kujua

Takriban asilimia 80 ya wanawake huathiriwa kwa wakati mmoja na tatizo la fibroids  au uvimbe katika ukuta wa mfuko wa uzazi . aiwapo una tatizo hilo unafaa ufahamu kwamba hauko pekee yako kwani wengi wanaathiriwa na fibroids wakati mmoja au mwingine . haya hapa yote unayofaa kufahamu kuhusu Fibroids kama  kama mwanamke .

1.   Hauko pekee yako . kuna wengi walio na tatizo hilo lakini hawana ufahamu kwa sababu ugonjwa huu hauna daalili kwa watu wengi . kuna uwezekano kwamba una uvimbe huo katika mfuko wa  uzazi bila kujua na hata ukawa nao kwa muda mrefu  uvimbe huo mara nyingi hauna hatari ya kusababisha kansa  lakini unaweza kufanya maisha kuwa machungu .

2.   Kuna aina moja tu ya fibroids ambayo huitwa majina kadhaa yakiwemo ;

.Leiomyomas

  • Myomas
  • Uterine myomas
  • Fibromas

Majina haya yote ni ya fibroids  ambao ni mkusanyiko wa uvimbe wa yama katika ukuta wa mfuko wa uzazi

3.  Fibroids  huja kwa size na shepu  malu mbali .

Kuna walio na uvimbe wa kiasi kidogo unaonekana kama matone ya mbegu  ambao hukuwamuda unaposonga na kisha kuhatarisha kubadilisha umbo la mfuko wa uzazi . kuna uvimbe ambao hukuwa mkubwa na kuwa misuli mirefu ya kuweza kushikilia uvimbe mwingine unaozidi kutokea katika mfuko wa kizazi .

Uvimbe ambao hukuwa  ndani ya ukuta wa kizazi huitwa  intramural fibroids.  Ilhali Submucosal fibroids hutoka nje ya upeo wa kizazi   na  subserosal fibroids  huonekana kutokea nje ya ukuta wa  mfuko wa kizazi .

4.   Uvimbe wa fibroids wakati mwingine hauwezi kuonyesha daalili .

baadhi ya wanawake huwa hawana daalili za fibroids  na hushangazwa wkati vipimo vinapoonyesha kwamba wana uvimbe huo  . kulingana na uliko uvimbe huo ,wakati mwingine inawezekana kuhisi mamumivu ya fibroids unapofanyiwa vipimo vya sehemu inayokaribiana na  tumbo .

Hata hivyo wakati mwingine kuna uwezekano wa kupatwa na matatizo  ambayo hayana uhusiano na uvimbe wa fibroids .Daalili za baadhi ya matatizo kama hayo ni pamoja na ;

  • Kutoa damu nyingi wakati wa hedhi .
  •  Hdhi inayodumu zaidi ya  wiki moja
  • Uchungu au presha karibu na tumbo
  • Kwenda haja ndogo kila mara na kupata matatizo kuachilia mkojo kutoka kibofu cha mkojo
  • Kuvimbiwa tumbo
  • Maumivu ya mgongo au miguu

Fibroids  inaweza kusababisha  uvujaji wa damu nyingi inayowza kukutia katika hatari ya kupatwa na maradhi ya  anemia.  Uvimbe mkubwa wa fibroids pia unaweza kuvuruga umbo la  mfuko wako wa uzazi na kufanya kuwa vigumu kulea mimba .

Pia utapata ugumu wa kushika mimba endapo uvimbe huo utaziba  kibomba kinachounganisha  mfuko wako wa uzazi  au kuathiriwa maumbile ya mfumo wako mzima wa  uzazi .

5.   Unafaa kufanyiwa vipimo vya kufahamu iwapo una fibroids na kujua kiasi cha uvimbe huo endapo utapatikana kuwa nao.

6.  Watalaam wangali hawajafahamu kinachosababisha fibroids   ingawaje kuna vichochezi  ambavyo huchagia ukuaji wa uvimbe huo katika mfuko wa uzazi .hivyo ni pamoja na

 Historia ya fibroids katika familia

  • Kuanza heshi mapema .
  • Unenepaji
  • Lishe yenye kiasi cha juu cha nyama na kiwango kidogo cha maboga
  • Pombe

7.   Muundo wa ukuaji wa fibroids hutofautiana kutoka mtu mmoja hadi mwingine . ukuaji unaweza kufanyika pole pole au kwa haraka .wakati mwingine kiasi cha ukuaji huo kinaweza kusalia vivyo hivyo kwa muda mrefu ,na baadaye kupotea au kupungua.Kuna uvimbe mwingine wa fibroids ambao hutoweka  baada ya uja uzito . Pindi unapokaribia menopause ndivyo hatari yako kupatwa na fibroids inavyopungua

8.  Kuna njia kadhaa za kutiu fibroids ikiwemo inayojulikana  kama    hysterectomy  ambapo uvimbe  sehemu au  mfuko wa uzazi wako huondolewa .

Mafanikio  katika teknolojia ya matibabu pia yamerahisha matibabu sasa kwani kuna njia za kukabiiana na uvimbe huo mapema bila kufanyiwa upasuaji . Tiba hizo ni za kupunguza uvimbe huo lakini sio wa kuumaliza kabisa . iwapo fibroids zinaathiri uwezo wako wa kupata mimba ,kuna upasuaji unaofanyika kuondoa uvimbe huo bila kuathiri mfumo wa uzazi .