Sudi ajisalimisha kwa polisi mjini Eldoret

Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi hatimaye amejisalimisha katika kituo cha polisi cha Langas mjini Eldoret asubuhi ya leo.

Hii inajiri siku moja baada ya polisi kukita kambi nyumbani kwake ili wamkamate kwa madai ya kutamka matamshi ya chuki na uchochezi.

Sudi atasafirishwa hadi Nairobi ambapo atafishwa katika afisi za NCIC (National Cohesion and Integration)

Mbunge huyo anakumbwa na mashtaka ya uchochezi na matamshi ya chuki.

"Jinsi nilivyotumiwa maafisa wa polisi kwangu nyumbani. Wakti walikuja kwangu sikuwa. Asanteni sana kwa kusimama nami," Sudi alisema.

Sudi aliandamana na wabunge Didmus Barasa, Caleb Kostany, Cornelius Serem, Gavana Stephen Sang na mwakilishi wa wanawake wa kaunti ya Uasin Gishu Gladys Shollei.