23 zaidi wapatikana na COVID 19 na kufikisha jumla ya watu 672 walio na virusi hivyo nchini

Watu 23 zaidi wameptikana na virusi vya corona na kufikisha idadi ya walio na ugonjwa huo nchini  kufikia 672.

Katibu wa utawala wa wizara ya Afya Rashid Aman pia amesema  taifa leo limesajili idadi kubwa zaidi ya watu waliopona ugonjwa huo baada ya watu 32 kuruhusiwa kwenda nyumbani na kufikisha 239 idadi ya waliopona ugonjwa huo .

Sampuli 1056 zimepimwa katika saa 24 zilizopita huku wakenya 22 wakipatikana virusi vya corona ilhali 1 ni raia wa Burundi . Hadi kufikia sasa sampuli 32,097 zimepimwa . Nairibi ina visa 4 ambavyo vipo katika mitaa ya Umoja (2) Komarock(1) na Pipeline(1). Mombasa imesajili visa 12 ,Mandera 6 na Kajiado 4

Aman pia ametangaza kwamba watu wawili zaidi wameaga dunia kutokana na ugonjwa huo  na kufikisha 32 jumla ya waliofariki kutokana na  virusi vya corona .