Guyo

Abdi Guyo asema maisha yake yamo hatarini, aeleza sababu

“Maisha yangu yamo hatarini”.

Hayo yalikuwa maneno ya kiongozi wa wengi katika bunge la kaunti ya Nairobi, Abdi Guyo.

Guyo ambaye alirekodi taarifa katika makao makuu ya DCI  siku ya Jumatatu, aliwaelezea waandishi wa habari kwamba anahofia usalama wa maisha yake.

Hii ilikuwa baada ya machafuko ambayo yalitokea kwenye mkutano wa kaunti wiki uliopita kufuatia kurudi kwa spika wa bunge hilo Beatrice Elachi bila kutarajiwa.

Je, Mariam Kighenda alipanga kujitoa uhai? Mmewe John afunguka

 Katika mkutano huo, kulishuhudiwa fujo ambapo meza na viti vilivunjwa.

Akiwahutubia wanahabari, Elachi alisema kuwa wanawake katika bunge la kaunti hilo wamechoshwa na vitisho.

Guyo kwa upande wake alieleza kuwa fujo ambao ulitokea ulikuwa umepangwa ili kuvuruga mkutano huo.

Tangu wiki ambayo mkasa huo ulitokea kuisha, amekuwa akipokea maandishi ya kutishia maisha yake.

Vile vile anadai kuwa watu wasiojulikana wamekuwa wakimfuata.

Mkimbia uchi usiku asimulia siri za familia anazotembelea,ajisifia kwa mbio

Photo Credits: courtsey

Read More:

Comments

comments