Afisa wa polisi wa kike azuiliwa kwa kujaribu kumuua mumewe

Afisa wa polisi wa kike anaendelea kuzuiliwa katika kaunti ya Kisumu kwa tuhuma za kujaribu kumuua mumewe kwa kumpiga risasi baada ya kuwa na mtafaruku baina yao.

Maureen Awuor anamtuhumu mumewe kwa kumpa mfanyakazi wao wa nyumba shilingi 50 bila ya kumjulisha.

Kamanda wa polisi Kisumu Mashariki Mwenda Musyimi amesema Awuor ambaye ni mshukiwa alimpiga risasi mumewe upande wa kushoto wa sikio lake.

Kulingana na taarifa, Awuor alirejea nyumbani kwao Nyalenda na kumpata mumewe akitazama runinga na kutoa bunduki aina ya AK47  na kutishia kujitoa uhai baada ya kumpiga risasi mumewe

Kwa sasa, mume huyo amepelekwa katika Hospitali ya Kisumu ambapo anaendelea kupata matibabu.