Afya Njema: Mboga hupunguza athari ya Kansa, Mshtuko wa moyo

Food
Food
Magonjwa hatari kama vile kansa na ugonjwa wa kisukari yanachangiwa na lishe duni.

Hivyo basi, kuna umihimu wa kuhamasisha Wakenya kuhusu vyakula vya asili ambavyo havina  madhara mengi katika afya ya binadamu.

Ulaji  mboga kwa wingi husaidia kupunguza maradhi ya kansa, ugonjwa wa kisukari na ugonjwa wa mshtuko  wa moyo.

Kila mwaka Oktoba 16, ni siku ya Vyakula ulimwenguni na kauli mbiu wa mwaka huu ni kuzingatia vyakula vya kiasili ambavyo vilikuzwa na babu zetu.

Vyakula hivi vya kiasili vimesekana kuwa muhimu sana katika maisha ya bindamu kwa kuwa vinakuzwa katika hali mazingira asili pasi na kemikali nyingi .

Kumekuwa na athari ya ukosefu wa chakula kutokana na kupuuzwa kwa vyakula asili na kutegemea vyakula vinavyokuzwa katika mazingira yenye kemikali nyingi.